Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, January 19, 2013

Pants on the ground/ijue historia ya uvaaji wa milegezo

Ijue historia ya uvaaji wa milegezo






kinadada tujirekebishe wengi wenu hata mambo yetu yale huwa mnayaonyesha(shanga na cheni za kiunoni)

 

Ninayofuraha kubwa leo katika safu hii ya urembo kuzungumzia suala hili la uvaaji wa milegezo kwa vijana wetu wa kiafrika.Nimeandika mada hii Kutokana na wasomaji  kuomba  sana makala hii,tunaambiwa kuwa uvaaji wa mwanaume au mwanamke hudhiirisha umri wake,Kuna baadhi ya mavazi ambayo ukimuona mtu kavaa bila kuuliza utajua tu huyu ni mtu mzima na ndiyo sababu ukimuona bibi kavaa mitindo ya mabinti wa sasa ataitwa bibi kijana au mzee kijana.Nakubaliana na hili kuwa uvaaji wa suruali wa mwanaume huendana na umri alio nao, wakati vijana wengi hushusha suruali zao chini ya makalio  huku wanaume wanaoanza kuzeeka huzipandisha suruali zao juu ya kiuno.

Binafsi naona kuwa  kuna uhusiano wa uvaaji wa suruali wa mwanaume na umri wake.Jaribu kuchunguza watoto chini ya miaka 12 kawaida huvaa suruali zao kwenye usawa wa kiuno kwakuwa  umri huo hununuliwa nguo na wazazi wao na wakati mwingine kuvalishwa na wazazi wao.Sasa kijana anapo kuwa tayari amekuwa(amebalehe) ndipo muonekano wake wa uvaaji unabadilika na kuanza kuvaa milegezo au kata K kama wanavyoita mtaani.
Leo mpenzi msomaji wa safu hii nataka nikujuze tu ili uweze kujua uvaaji huu umetoka wapi?.Hapa Tanzania mtindo huu hujulikana zaidi kama  kata K au mlegezo na  vijana wengi  wanaopenda kuvaa nguo za ndani maarufu kama  Boska(Boxer) au kaptula hushusha suruali zao chini ya makalio,mimi huwa sielewei kwamba tatizo huwa nini? au wenzetu mnaogopa kubanwa viuno vyenu na mbaya zaidi nguo wanazozionyesha huwa chafu na mda mwingine huwa na maandishi mabaya(cow boy) na zaidi zingine mpaka bei yake huwa mbovu nikimaanisha bei ya chini.

Mtindo wa mlegezo uliigwa kutoka mfumo wa magereza nchini Marekani ambako mikanda ilipigwa marufuku katika magereza ili kuzuia wafungwa kujinyonga. Lakini mtindo huu ulikuja kupewa umaarufu na wasanii wa muziki wa hip-hop katika miaka 1990 na tangu wakati huo umekuwa kama alama ya uhuru na utambuzi wa kitamaduni au alama ya kukataa maadili ya jamii.Jaribu kukumbuka kuanzia bongo flava ilipo anza hapa Tanzania vijana wengi waliokuwa wakiimba bongo flava na wanafunzi  walipendelea kuvaa milegezo kutokana na kuwaiga wasanii wa hip hop wa Marekani na kusahau maadili na utamaduni wetu kama Watanzania ingawa tatizo hili lipo  hadi sasa, kuna vijana ambao hawawezi kuacha kuvaa milegezo.
Naomba ni mnukuu kijana Elias mkazi wa Arusha   anazungumziaje? suala hili la uvaaji wa milegezo" kiujumla mimi wana ni kera na siku moja nilikuwa katika daladala  na konda wa daladala aliinama mbele yangu nguo chafu  huku suruali ikiwa chini ya makalio  nilichokifanya nilimpandisha suruali kisha nika mwambia vaa vizuri bwana unavaavaa vibaya halafu unaniinamia watu kwenye daladala walikaukia kucheka na konda hakushusha tena suruali yake mpaka tumefika "Ninachojaribu kukisema hapa  ni kwamba naomba tubadilike kama mnavyo wazungumzia watoto wa kike na mavazi yao kuwa yanakwenda kinyume na utamaduni wetu hivyo hivyo kwenu nyinyi wanaume haipendezi ukiwa una tembea njiani au umeongozana na mama,bibi,baba hata mchumba wako  na unaona kawaida tu kuvaa hivyo kiukweli hapendezi naomba niifanananishe uvaaji huo na muonekano wa makalio ya nyani kama kijana  badilika ,ukivaa vizuri utaonekana mstaarabu daima hata kama unafanya biashara watu watavutia kutokana na uvaaji wako bila kuwa sahau dada zangu mnao vaa blauzi fupi na mkiinama nguo zenu za ndani zionekana naomba tuhistili miili yetu vema .

Mpenzi msomaji usichoke kuendelea nami katika safu hii kuanzia wiki ijayo nitaendelea kukupa mada mbalimbali za urembo na mitindo,wiki hizi mbili tulikuwa tunawekana wazi katika suala zima la uvaaji kwa upande wa wanaume na wanawake.


abnerytupokigwe@gmail.com

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu