Enter your keyword

Culture for Life.

Friday, January 11, 2013

MAVAZI YANAVYOELEZEA TABIA YA MTU


leo nataka tukumbushane katika suala hili la mavazi ambalo kila mmoja wetu anatambua umuhimu wa mavazi katika maisha yetu ya kila siku.Kuna namna mbalimbali ya uvaaji kulingana na dini ya mtu,kabila pamoja na Kazi ni kiwa na maana nzima kuwa mavazi tunayovaa siku zote hutegemea mazingira tuliyopo kulingana na chaguzi ya moyo wako kuwa unapendelea mavazi ya aina gani?.

Lengo langu  hasa leo kuzungumzia suala hili la mavazi na tabia ya mtu nikutokana na kero kubwa niliyoiona mtaani kwa upande wa wasichana pamoja na vijana wa kiume  wanapokuwa mada na kujadiliwa na watu  wanapotazamwa  mavazi walio vaa.Ninapozungumzia  suala  hili la mavazi kuwa huakisi tabia ya mtu,ninamaanisha kuwa muonekano wa mtu ndani ya vazi fulani linaweza kukujulisha kuwa mtu huyo anatokea katika mazingira gani?,hali yake ya  kiuchumi na utaweza kutambua kuwa anafanya kazi gani? na amelelewa katika malezi gani? kulingana na vazi alilovaa.

Hapa na zungumzia pande zote mbili wanaume pamoja na wanawake kuwa katika uchaguzi wa mavazi inatupasa kuwa makini ili kulinda utamaduni wetu kama Watanzania na pia wazazi tuwe makini tunapowachagulia watoto nguo toka wakiwa wadogo.Ilikuwasaidia baadaye wasiende kinyume na maadili ya utamaduni wetu.

Ningependa nianze kuelezea  suala hili la mavazi kulingana na mazingira,watu tunashindwa kutofautisha mavazi ya ofisi,michezo,disko,sherehe na mavazi ya kulalia.Nianze na dada zangu kwa kweli kuna mavazi yameingia siku hizi tunaita skinitaiti(skintight) ambazo hufaa kuvaliwa na blauzi ambayo ni ndefu lakini dada zangu tumefanya nguo hizo kama suruali bila kujali miili yetu inaonekana vipi? ndani ya mavazi hayo.Hata kama tabia yako ni nzuri ukisha vaa hivyo unaonekana kama changudoa kama mtu anae nadi mwili wake tubadilike na tuepuke kudharirishwa huko mitaani,nasema hivi kwasababu nimeshuhudia dada mmoja akichaniwa nguo ya aina hiyo stendi na wanawake wenzake walipo jaribu kumpa kanga vijana hawakukubali zaidi waliendelea kumtoa nguo zingine.Tafadhari tubadilike nguo zingine hazi stahili machoni kwa watu kuacha kuvaa hivyo basi jitahidi uvae nguo hizo usiku.


Pia watu wengi wanaiga mavazi kutokana na Utandawazi huu tulio nao sasa mavazi wanayo vaa wenzetu ni kutokana na mazingira yao yalivyo sasa sisi wabongo tunaiga na kuvaa nguo kama zao mfano nyakati za baridi mtu kavaa blauzi nyepesi mikono wazi chini kavaa kaptula fupi au sketi fupi na wala hajali.Kwahiyo tabia ya mtu inaweza ikaonekana kutokana na mavazi yake hujiulizi kwanini watu husema huyu katoka kijiji huoni hata anavyo vaa,au huyu mmasai kutokana na aina fulani ya nguo sitaki kusema ni aina gani ya nguo wanapenda wamasai au kabila lolote lile wenyewe tunafahamu.

Hali ya uchumi, hapa wengi tunajitahidi kuuficha umaskini katika mavazi  ingawa wengine huwa kinyume hata kama anapesa utamkuta yupoyupo tu.Hiyo inakuwa tabia ya mtu kutokujijali.Naomba niseme kuwa binadamu tumeumbwa tofauti hilo tukubali lakini ni vema zaidi ukiwa unapendeza mda wote sio lazima ujionyeshe kwamba huna ,kile ulicho nacho kitumie ndipo utapata kingine.

Mwisho kabisa napenda kusema kuwa tabia ya mtu si mavazi watu wengine wanaweza kuvaa vizuri,na kuwa na tabia nzuri n'je kumbe ndani hawafai pia wapo wanaotumia mavazi kuwalaghai watu huko mitaani.Hivyo basi tuwe makini pia kaka zetu mazoea ya  kuvaa milegezo tupunguze.


abnerytupokigwe@gmail.com






No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu