Historia fupi ya muziki wa kizazi kipya
ulianzishwa na Wamerekani weusi huko the Bronx, New York Marekani mnamo mwaka 1970.Wamerekani wenye asili ya Afrika ,ambao babu zao walichukuliwa kwenda Marekani kama watumwa.Elementi hizi za utamaduni wa hiphop zilikuwa zikijitokeza kwa awamu moja na inapofifia inaibuka nyingine ,ilivyo ni kwamba ilianza grafiti ikafuatwa na udijei,mabreka,halafu rap(yasin,2001;rose1994;toop2000;mitchel2001;southern1983).
Mizizi hasa ya rap Afrika, mbali ya kuanzishwa na wamarekani weusi una sifa mbalimbali za kimuziki na kifasihi simulizi za kiafrika ikiwa ni pamoja na matumizi ya midundo au ridhimu usimulizi,kiitikio na majigambo.Hiphop au muziki wa kizazi kipya ulikuwa kama jukwaa la mshikamano miongoni mwa vijana wa kimarekani wa mjini na baadaye kuwa kama mtindo wa maisha na sauti ya vijana .Ni utamaduni ambao uliwakutanisha wale walionyimwa haki ,walionyanyaswa na kugandamizwa katika historia na ukawa utambulisho miongoni mwa Wamerekani weusi na ukawa kipaza sauti chao.
Muziki wa kizazi kipya au rap nikipengele kimoja wapo cha utamaduni wa hiphop.Ni aina ya ushairi ,usimuliaji,au usemaji unaopangwa vina kwa kufuata mdundo wa ala za muziki (ambao tayari ulisharekodiwa ).Muziki huu ulianza kama sehemu ya burudani ya vijana weusi na baadaye ukakuwa na kuenea na kuwa maarufu katika nchi nyingi duniani .Hapa Tanzania muziki wa kizazi kipya ulianza mwaka 1980.Vijana walianza kuimba wakiwa ufukweni na baadaye katika sherehe mbalimbali ulianza kisikika redioni mwaka 1995.
Kama ilivyokuwa kwa Wamerekani weusi vijana wengi wa Kitanzania pia hutumia muziki wa kizazi kipya kuelezea matatizo yao ya kila siku kama vile ukosefu wa ajira na athari zake ,Dola na nguvu zake na umasikini.Hapo mwanzoni nyimbo hizi ziliimbwa kwa kuwaiga wasanii wa kimarekani kama vile Vanillah Ice,Kriss Kross na Naughty by Nature, halikadhalika walitumia baadhi ya maneno au sentensi kutoka nyimbo hizo .Hivyo kila mwimbaji alijaribu kuwa mbunifu na kutunga nyimbo zake mwenyewe ilikuwapata mashabiki na kujiongezea umaarufu.Muziki wa kizazi kipya unaojulikana sana kwa jina la Bongo flava ulishika kasi sana mwaka2000.muziki huu umewapatia vijana wengi fusra baada ya kusikia nyimbo kutoka n’je ya
Tanzania hususani marekani ambapo vijana waliiga na kutoka na staili yao wakitumia lugha ya Kiswahili na wengine walichanganya nyimbo hizo na lugha kama Kingereza na lugha za asili.
Walichoweza kufanya vijana wengi ni kuiga (ala) za Wamerekani lakini waliamua kutumia lugha ya Kiswahili ili kuweza kufikisha ujumbe kwa Watanzani na kama inavyojulikana kuwa kazi yoyote ya sanaa ina malengo ya kufundisha ,kukosoa na kuburudisha.Wakati muziki huu unaanza Tanzania hakuweza kuzaniwa kama unge fika karne za mbele lakini hivi sasa una waimbaji wengi pamoja na mashabiki wengi wa rika tofauti hasa vijana, watu wazima si wote wanao upenda muziki huu.
Baadhi ya vijana waliokuwa waanzilishi wa muziki huu kwa Tanzania,vijana wa mwanzo kabisa ambao kuanzia mavazi yao na kufokafoka kwao kulikuwa ni burudani tosha kwa watu kuanza kudadisi kuhusu utamaduni wa mavazi hayo ambayo yalionekana kama uhuni tena wa kupita kiasi kutokana na uvaaji wa mavazi hayo kihip hop.Hawa ni baadhi ya wasanii wachache ambao walivaa kihip hop Samora Avenue,John simple,DJ Rusual,The BIG ONE,Babu manju,Davidi,Nhigula,Abdulhakim Magomelo,Kessy,Ibony Moalim,Tom
London,Opp(now JayP) NA DJ Ngomeley.Hao walikuwa chachu katika uvaaji wa kihiphop na katika kughani Muziki huu wa kizazi kipya.
Pia kuna wasanii wa mwanzo kabisa katika kuimba muziki huu wa kizazimkipya akiwepo mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (BBG lianza na MR.11)FreshXE Mtui,Adili Kumbuka,KBC(Mbeya Tech)Saleh Jabir,Samia X,The Big,Rhymson,2Proud,Kwanza Unit,GWM,Hard Blasters na Bantu pound ambao walianza kuimba katika sherehe za mashuleni,kwenye matamasha mtaani kabla hata ya kurekodi nyimbo zao studio. Kulikuwa na wale wenye kuimba kama wanamuziki wengi wa Marekani kwa kupitia matamasha mbali mbali katika Jumba la utamaduni la Urusi,Korea na mengineyo yaliyokuwa yakiandaliwa hasa na wanafunzi wa shule mbali mbali za sekondari jijini kama Forodhani pia matamasha yaliyokuwa yakifanyika kando kando ya ufukwe ambako wengi wenye kutaka kuimba walijitokeza.
Kulikuwa na kundi kama la Mawingu na mwana dada Pamela,mwanadada Stara Thomas na Judith Wambura ambao uwezo wa kughani na kuimba kama Mc Lyte ulimuinua hasa alipofanya hivyo kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha DJ show ya Radio One,shukrani kwa Ipyana Malecela Mkwavi (RIP) kwa zawadi ya LP yenye mdundo,ala ya single “Keep,Keeping on” ndiyo iliyomtambulisha Jay Dee wa leo Radioni kwa mara ya kwanza japokuwa kabla ya hapo alikuwa mwimbaji wa kwaya kanisani lakini mweye kusita kuingia kwenye muziki wa kidunia.
Pia Kundi la R&B lililojulikana kama Four Krewz Flava pia Herbert Makange ambaye pia alikuwa akiimba. Kwa kufanya haya na mengineyo mengi muziki huu sio tu utakuwa ni wenye kujijengea heshima bali kuweka kumbukumbu kubwa ya mapinduzi kwenye ulimwengu wa muziki Tanzania na hadhi yake kuwa ni ile isiyofutika kwa urahisi machoni na akilini mwa kizazi cha sasa na hata kile kijacho kwa muda mrefu.
Maisha : Kurejea kwa Toto Afya Kadi Mwanga Mpya Bima ya Afya - Mhagama
-
Na WAF, DODOMA
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema kurejeshwa kwa Toto Afya Kadi
kutaleta matumaini mapya na uelekeo thabiti wa Bima ya Afya hus...
1 day ago
No comments:
Post a Comment