JUMPSUIT(Bwelasuti) na uvaaji wake.
Mpenzi msomaji wa safu hii ya urembo na mitindo ya mavazi leo nataka kuwajuza historia ya vazi hili ambalo kwa sasa limekuwa likivaliwa sana katika mandhari mbalimbali.
Mtindo huu Jumpsuit unaweza ubadilisha badala ya kuvalia suruali pia unaweza kuvaa na skirt fupi au kigauni kifupi na high heels. |
Bwela suti au ovaroli(Jumpsuit) mwaka 1960 ni vazi ambalo zamani lilitumika sana na watu wanaoruka na parachuti kwa lengo la kuzuia hali ya baridi na upepo.
Mwaka
1987 vazi hili lilipata umaarufu katika sekta mbalimbali ambapo
lilianza kuvaliwa na Marubani,madereva,wanamichezo,Mafundi bomba,mafundi
mitambo,Wasanii pia huvaa jukwaani, huku vyuoni/mashuleni likivaliwa kama sale katika vyuo vya ufundi.
Wazazi wengi huwavalisha bwelasuti watoto wanaotambaa kwa lengo la kuzuia baridi pia kuhofia kuchafuka kwa wale walio katika kipindi cha kutambaa.
Hicho kibwebwe cha nyuma waweza shona kwa style ya kukitoa,unakuwa na uwezo wa kuivaa nguo moja katika muonekano tofauti. |
Vazi hili limeendelea kushika nafasi kubwa katika swala la mitindo huku wabunifu wengi wakibuni vazi hili katika mitindo mbalimbali.
Jinsi ya kuvaa bwela suti
1.Tambua kiuno chako
Hakikisha unajua kipimo cha kiuno chako wakati wa kuchagua bwelasuti iliyo sahihi.Lazima rastiki au mkanda uliopo katika bwela suti ushike vema kiuno chako ili kuepusha muonekano mbaya wa umbile lako .
2.Fanya chaguo sahihi la bwela suti kulingana na umbo lako
Nivema
kutambua umbo lako ili kuweza kuonekana nadhifu ndani ya vazi
hili.Kwanza kabisa kwa wale wenye miguu mrefu ni vema kuvaa bwela suti
ambazo ni pana miguuni,watu wafupi au wenye urefu wa wastani hutakiwa
kuangalia aina ya kitambaa na urefu wa vazi hili.
Wenye
maziwa madogo,mikono miyembamba lakini wamejariwa nyonga(hips)
unatakiwa kuvaa bwela suti yenye muonekano wa blauzi zaidi pia iweze
kuonyesha mikono yako vizuri.hii itazuia muonekano wa nyonga zako zaidi.
3.Vaa bwela suti na koti
Watu
wengi huofia kuvaa bwela suti kutoka na mitindo mbalimbali ya vazi hili
kuonyesha mabega,mgongo na sehemu kubwa ya mikono.Kama wewe ni mmoja
wapo jaribu kuvaa vazi hili na koti,utaonekana nadhifu pia litakuzuia
baridi na kuficha mikono yako ni vema koti liwe fupi ili kuonyesha umbo lako na mtindo wa bwela suti uliyoivaa..
4.Uchaguzi wa rangi za bwela suti
Bwela
suti yenye rangi moja huvutia zaidi kuliko bwela suti yenye rangi moja
juu na chini rangi nyingine au yenye mchanganyiko wa rangi mbalimbali
chini,Katika uchaguzi wa rangi wengi hutofautiana kulingana na chaguo la
mvaaji.
5.Uchaguzi wa kiatu cha kuvalia bwela suti
Unaweza kuvaa viatu vya chini(Flat shoes) au viatu virefu na bado ukaonekana mwanamke nadhifu na mwenye kuvutia zaidi bila kujali umri ulionao wala umbo lako.
No comments:
Post a Comment