Enter your keyword

Culture for Life.

Tuesday, December 13, 2016

Penzi la Dhati huleta baraka katika Ndoa.

By On December 13, 2016


Sara anasema" Katika kila jambo ni vema  kumuweka Mungu mbele kwani hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea just blv in God."

Sara Issa ni miongoni mwa warembo wanaonivutia katika ukurasa wangu wa facebook,Napenda sana mtu anayependeza,Dada huyu anajipenda sana na naweza sema ni mrembo,anajitambua na kujithamini.Kutokana hilo siku sita kufanya naye mahojiano kwa njia ya facebook massenger.Kama ifuatavyo:

 

 

 

 

 

 

 


 

 

Jina:Sara Issa.

Umri:30

Mkazi:Arusha.

Uraia:Mtanzania

Mahusiano:Nimeolewa 



 {Mahojiano kati ya Sinyatiblog na Sara Issa siku ya tarehe 12/12/2016 kupitia facebook messenger}

SINYATIBLOG:Ni rangi gani unapendelea katika mavazi yako
SARA ISSA: Colour ninayopenda sana ni red ata kwangu rangi kubwa iliyotawala ni red bt kwa mavazi napenda zile zinazonifanya kuwaka.

Napenda Rangi Nyekundu.


SINYATIBLOG:Nini siri ya unadhifu wako.
SARA ISSA: Ok unadhifu wa mtu upo ndani ya mtu na huwez kuiga bt unachoweza ni kujifunza.mm napendaga kuwa unique ck zote yaàn nina wish siku moja niwe mtu fulani tofaut bt cjajua ndoto yangu itatimia vp napenda kuwa tofaut cpend ,yaaan kufanana sehemu na mtu always napenda kuwa smart na ugonjwa wangu kunukia kubeba handbag nzur .

"Napenda viatu virefu kwasababu mimi ni mfupi",Nikweli viatu virefu huongeza mvuto kwa mwanamke yeyote yule,nakumfanya aonekane smart.


 SINYATIBLOG: kitu gani kinakuvutia upande wa vitu vya asili katika muonekano wako wa mavazi,
ambacho unapenda Zaidi.
SARA ISSA:Napenda kushona nguo za vitenge sana, napenda kuvaaa viatu virefu sana coz mm ni mfupi pia napenda sana kushona magauni mapana yawe ya kitenge au another material napenda nguo fupi pia bt hapa kwa fupi,nyingi zinakuwa za mtumba au madukani.

"Napenda sana Pochi"


SINYATIBLOG:Asante Sana Sara, swali la mwisho una ushauri gani kwa watu wasiopenda vitu vya asili.
SARA ISSA:Vitu vya asili ni vizuri kuna mwingine anaweza sema havipendi bt kumbe ata hivyo vya dukani hapendez ,kinachotakiwa ni kujijua tu ww na mwil wako na nn unapendeza ukivaaa na unavutia hakuna mwenye mwil mbaya ni vile kujielewa na kujikubali ww mwenyewe.



SINYATIBLOG:Sara una ushauri gani kwa dada ambao bado hawajaolewa pia una waambia nini wanaume ambao husema nipo nipo kwanza  huku  wakiwa wako tayari katika mahusiano  ya mda mrefu na wenzi wao.

MR &MRS..ALILOPANGA MUNGU MWANADAMU HAWEZI PANGUA.



SARA ISSA:Ili la kuoa au kuolewa ni gumu bt ninachoweza kuwashauri ni kwamba mwisho wa siku family matter.tutafanya yote tutafanya starehe bt cku ya cku family inahitajika.kuna kipind kwa sisi wadada unataman familia sana hivyo bila kufanya maamuz au kuchukua hatua hakuna kinachosaidia.na kuhusu kukaaa sana ktk mahusiano sio ndio guarantee ya kuoa au kuolewa mpnz japo mm alienioa nilikutana nae shule unaweza kaaa na mti cku chache akakuoa na ukakaaa na mtu miaka kenda na hackuoe kinachotakiwa ni maamuz tu upendo na uvumilivu and blv mi pesa sio kila kitu pesa zinatafutwa ata hao wenye pesa wana historia nazo.kila kitu ni kumuweka Mungu mbele kwan hakuna jaribu liclo na mlango wa kutokea just blv in God.

Lulu katika vazi la vitenge.

 SARA ISSA:.kuna wadada wawil napenda da way wanavyovaaa lulu na wolper sana bt cna hela tu shoga bt najitahid kumanage kile ninachopata na kufanya nafc yangu iridhke napenda kupendeza napenda kuvaaa vizuri

Wolper katika Max dress.

 

SINYATI BLOG:Thank kwa ushirikiano Sara,naamini kuna watu  wamejifunza kitu kupitia haya mazungumzo tuliyo yafanya siku ya leo.Nashukuruu sana.

Monday, December 12, 2016

EATV Awards 2016."Wasanii waliopendeza na nakshi za kiafrika katika muonekano wao"

By On December 12, 2016

Msanii Mrisho Mpoto akifuatilia matukio,Nampenda huyu msanii ni moja ya wasanii wanaokubali kazi za Kiafrika.Picture credit:Othumani Michuzi.



Lady Jay Dee akipokea  Tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike .Picture credit:Othuman Michuzi.



Picture credit:Othumani Michuzi.

Picture Credit:Othumani Michuzi



Siri Usio Ijua Kuhusu Chumba Chako Cha Kulala.

By On December 12, 2016

Mito ni Pambo katika kitanda chako pia ni kitu ambacho wengine hupenda kuikumbatia hasa wakati wa baridi huleta joto.{si kwa watu wote}

Chumba ni sehemu muhimu kuliko mahali popote katika nyumba.Tulio wengi huona sehemu hii kama mahali pa kupumzika pale tunapokuwa tumechoka na wakati wa kulala ndipo huwa tunakumbuka eneo hili.
Fahamu kuwa hamna sehemu iliyo na maana sana katika maisha yetu kama chumbani au sehemu ya kulala.
Sehemu hii inapaswa kuwa tulivu, safi na yenye vitu  vichache, Unapoweka vitu vichache ndani ya chumba chako utakifanya kiwe na  hewa nzuri nzuri zaidi.
Chumbani  ni mahali ambapo unaweza kupumzisha ubongo wako na kufikiria mikakati   ya kimaendeleo na ukaweza kupata wazo jipya lakini yote hayo utayapata endapo chumba chako kitakuwa kisafi, tulivu pamoja hewa nzuri.

Zifuatazo ni dondoo za upambaji wa chumba:

Mwanga
Chumba kinapopata  mwanga wakutosha huvutia zaidi  na kuwa na hewa ya kutosha.
Ninapo zungumzia mwanga nina maanisha mwanga kutoka dirishani, mwanga wa taa za chumbani ambazo uwekaji wake upo tafauti kulingana na uwezo ulio nao, kuna taa ambazo huwekwa chini, ukutani au zile ambazo huwa pembezoni mwa kitanda. Mwanga wa taa ya chumbani hupaswa kuwa hafifu.
Rangi.
Katika uchaguzi wa rangi ni pamoja na rangi ya ukuta wa chumba chako, mapazia, shuka, pamoja na rangi za mito. Hapa inategemea unapendelea rangi gani lakini unashauriwa rangi za chumbani ziwe rangi ambazo ni tulivu.
Sehemu ya joto utatakiwa kuweka mapazia ambayo sio mazito, katika hali ya baridi tumia mapazia mazito pia ni muhimu kuzingatia rangi, usipendelee rangi zitakazofanya chumba chako kuwa giza.
Pendelea mashuka yenye rangi moja au yenye maua machache. unapaswa kutumia rangi ambazo huonyesha usafi mfano rangi nyeupe.
Unaweza kuchanganya na rangi zingine katika mito yako ya kitandani.Ubunifu katika utandikaji wa kitanda chako ni muhimu ili kiweze kukuvutia muda wote.
Sakafu
Kuna watu wanaopenda kutumia Mazulia (carpets) chumbani. Jaribu  kuchagua rangi nzuri aidha inayoendana na ukuta wako wa chumbani, ilikuleta muonekano mzuri pia unashauriwa kapeti lisiingie chini ya kitanda ili kukupa  urahisi wakati wa kufanya usafi.
Ni muhimu kusafisha zulia lako ili kuondoa vumbi na kuepuka kupata mafua. Pia ni vema kuwa na tabia ya kulitoa maramoja moja ili kuweza kusafisha sakafu yako na kuondoa harufu ya unyevunyevu  uliopo chini ya zulia.
Mwisho zingatia kuweka vitu vichache chumbani na kuwa na mpangilio mzuri wa vitu ndani ya chumba chako.

Njia za Kuepuka Chunusi Usoni, "Epuka matumizi ya vipodozi vyenye Kemikali"

By On December 12, 2016

Natumia Vaseline original,situmii vipodozi vyenye kemikali zaidi ya mafuta mgando usoni na lotion mwilini.Matumizi ya vitu vingi usoni husababisha sura  kuwa na mikunjo au kuchoka na kuonekana mzee.


Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama vivimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa . Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe Karibu asilimia 85 ya  vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na  zaidi ya  asilimia 20 ya wanawake  wenye umri wa zaidi ya miaka  ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.
Vipele vinaweza kuwa vidogo  au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu  mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa  ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni.
Chanzo cha Chunusi
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
Umri
Kama nilivyosema( hormone)vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubalehe.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa  nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
Vipodozi
Baadhi ya vipodozi vya usoni(Make-up) za kina dada na Marashi(spray) za nywele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
Chakula
Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufanya chunusi kuwa nyingi zaidi.Hasa vyakula vyenye mafuta.
Dawa
Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na makusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
Magonjwa
Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana
Mazingira
Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye  mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekano wa kupata chunusi.
Jinsia
Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
Familia
Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia  wa familia kadhaa kuliko nyingine.
Homoni
Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
Usafi wa mwili
Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele  husababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwilini au kutooga huongeza uwezekano wa kupata chunusi
Mawazo(Stress)
Mtu anapokuwa na mawazo mengi vikemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huweza kuchangia au kusababisha chunusi
Dalili za Chunusi
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo.
Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana Daktari kuzigundua,japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari  au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale vinapotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya  zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu, chakula,ngozi,dawa unazotumia na vitu vingine vinavyoweza.kuchangia mtu kupata chunusi
Matibabu
Matibabu ya chunusi yanajumuisha  kupunguza utoaji wa (sebamu ),kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingi au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyokwishakueleza katika makala iliyopita.
Dawa za kupaka
Kuna dawa za kupaka ambazo hupakwa katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi.Dawa hizi hupatikana kama cream,losheni,jel .Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu.
Dawa nyingine ni zile zinazolainisha nta  na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi  na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
.
Matibabu mbadala
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu na kuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu wenye chunusi wanashauriwa  kula mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi,matunda , mboga za majani,vitamin B. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa,tumbaku,sukari,vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi.
Mambo ya kuzingatia ili usipate Chunusi
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
·      Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi  kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu chochote kigumu.
·      Tumia  Vipodozi au vilainisha ngozi visivyo na mafuta  ya mgando
·       Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
·      Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
·      Usibinye au kutoboa  vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
·      Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
·      Punguza mawazo

Kumbuka kuwa chunusi haziwezi kutibika kabisa   iwapo matibabu yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona  na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwe na madoa kwa nija ya kiasili, njia zifuatazo zaweza sana kukusaidia.Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainika changanya na asali, paka usoni.Ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilika kwa kipindi kifupi.
Kama utashindwa kupata vitu hivyo tafuta sabuni pamoja na krimu yenye mchanganyiko wa asali na ukwaju,lakini nadhani asali na ukwaju kama utaenda sokoni ni rahisi kupata.Pia ni vema ukitumia losheni yenye mchanganyiko wa asali au ukwaju.

Jinsi ya Kuvaa skafu "Shanga Skafu"

By On December 12, 2016
 Katika safu hii utaweza kufahamu na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu urembo na mitindo ya mavazi kwa wanaume na wanawake, na hivyo kukufanya msomaji kwenda na wakati na kuonekana wa kisasa zaidi.
 Katika makala hii ya mwanzo kupitia safu hii nitajikita katika kuzungumzia juu ya uvaaji wa skafu pamoja na kukujuza mavazi yanaoendana na skafu.
Kwa kuanza kabisa napenda utambue kuwa skafu ni kitambaa kinachovaliwa shingoni kama urembo, unaweza kuvalia na aina yoyote ya nguo kwa kuzingatia muktadha na vazi unalovalia.
Kuna aina mbalimbali za skafu kutokana na aina ya kitambaa pia ukubwa na muundo wa skafu, mfano kuna skafu ndefu, fupi na nyingine zamraba.

Skafu hizi zimetengenezwa kwa kutumia shanga mchanganyiko, ni rahisi sana  unaweza kuzitengeneza hata unapo kuwa nyumbani.


Katika Miji mbalimbali yenye hali ya baridi, imekuwa kawaida sana kuwaona vijana na watu wengi, wanawake na wanaume wakiwa wamevaa skafu kwani ni moja ya vazi linalomfanya mtu aonekane nadhifu na kupendeza zaidi.

Kuna njia tofauti za kufunga skafu, na hii mara nyingi hutokana na aina ya nguo mtu aliyovaa pamoja na sehemu anayokwenda.

Unaweza funga skafu kwa kulinganisha pembe zilingane na pia unaweza kufunga katika nusu ya urefu, kisha kuiweka kwenye shingo yako ili mwisho moja iwe ndefu nyingine iwe fupi kufanya fundo huru katika pande zote.

Zile skafu ambazo zipo mraba unaweza kuikunja kwanza kama pembetatu kisha kuiweka shingoni huku ukiifungia nyuma ya shingo na ukaonekana nadhifu.
Skafu huvaliwa na wanaume na wanawake, ingawa mara nyingi wanawake ndiyo wenye uwanja mpana sana wa kuvaa skafu. Skafu uweza kuvaliwa na nguo yeyote pia husaidia kuongeza mvuto wa vazi ulilovaa.
Sehemu za baridi mara nyingi utaona watu wakiwa wamevaa skafu ilikujikinga na baridi na kipindi cha baridi ni vyema ukitumia skafu nzito na ufungaji wake lazima uwe ule wa kuzungusha shingoni kama duara.
Licha ya skafu kuvaliwa shingoni, pia inaweza kutumika kama kibanio cha nywele na wengine wanazitumia kama mkanda, na pia unaweza kuifunga skafu yako pembeni ya mkoba wako ikiwa ujapenda kuivaa shingoni lakini hapa ni zile skafu fupi ambazo siyo ndefu ndiyo unaweza kuzifunga pembeni ya mkoba wako.

Skafu asili ,unaweza kuzivaa shingoni katika muktadha wowote .

 Unashauriwa ukivaa skafu usivae mkufu kwasababu hauwezi kuonekana na pia, ni vyema kuvaa skafu nzito kipindi cha baridi na wakati wa jioni, mchana unashauriwa kuvaa skafu ambazo ni nyepesi kulingana na hali yahewa itakavyo kuwa.
Ukiwa umevaa vazi la Ofisini pendelea kuvaa skafu fupi kulingana na vazi ulilo vaa.
MWISHO…

Siri 5 Zinazomfanya Mwanamke Kuwa Moto Wakati Wote.

By On December 12, 2016
Kuna msemo usemao kuwa “mwanamke ni pambo la nyumba”hivyo basi kama mwanamke ni pambo la nyumba ndani hata n’je pia  unastahili kuwa nadhifu.Leo katika safu hii ya urembo na mitindo nitazungumzia vitu vichache ambavyo vitakusaidia wewe mwanamke bila kujali kipato chako cha uchumi. 

Bloggers wanawake katika picha ya pamoja siku ya tarehe 5/12/2016 katika mkutano mkuu waTBN,uliofanyika ukumbi wa Golden Jubilee tower jijini Dar es Salaam.Picture credit:Othumani Michuzi.

Kujiamini na kujikubali 

 wanawake wengi hushindwa kuvaa baadhi ya mavazi kutokana na maumbile yao,Huona  kuwa miili  yao haiwezi kupendeza katika  mavazi mengine.Mfano wapo watu ambao hushindwa kuvaa nguo fupi kutokana na kuona kuwa miguu yao ni mibaya.Unapaswa kuujua mwili wako  na  mavazi ambayo yanakupendeza na kukuonyesha nadhifu,kwa watu wanene ni vema kuvaa nguo ambazo nipana nikiwa na maana kuwa zisichore mwili wako na kutengeneza muonekano mbaya.Wale wembamba wao wana uhuru katika mavazi isipokuwa usipo jitambua utaonekana kituko uchaguzi wa vazi utakalo kuwa umevaa.

Tambua rangi ya nguo zinazokupendeza,

chagua rangi inayoendana na ngozi yako ambayo itakuonyesha vema,kuna baadhi ya rangi ukivaa zitakufifisha  na kukufanya uonekane ujapendeza hata kama vazi lako ni zuri na la thamani.

Panga bajeti  

kwaajili ya kununua vitu vyako vya msingi ni kimaanisha mavazi,heleni.bangili,mkufu,Hapa mwanamke unashauriwa kununua gauni jeusi,katika manunuzi yako, gauni jeusi fupi au refu,hili litakusaidia unapokuwa na mtoko au sherehe utaweza kutupia gauni lako na kuchanganya na heleni bangili au mikufu na utaweza kuvaa kwenye  mtukio tofauti na kuoneka mpya huku uikiwa umeficha umasikini.

Fanya mazoezi 

wanawake wengi hatuna kasumba ya kufanya mazoezi siku zote.Maozezi ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha viungo vyetu na kutengeneza muonekano wa mwili(body shape).Hii itakusaidia kuepuka matumizi ya dawa zakuongeza maumbile mfano dawa za kuongeza nyonga(hips) na makalio.

 Tumia Maji na Matunda 

ni muhimu kunywa maji angalau lita moja kwa siku kiafya,itakusaidia kuimnarisha ngozi yako,pia jitahidi kupata matunda katika mlo wako au unaweza kutumia matunda kama kifungua kinywa chako na kuepuka utumiaji wa vitafunwa vyenye mafuta.

Epuka utumiaji wa madawa ya kongeza maumbile,

kubadilisha ngozi nikiwa na maana ya vipodozi vya kuchubua mfano Carolight.Hivyo ni baadhi vitu vichache ambavyo ukizingatia mwanamke utaendelea kuonekana kijana na kuepuka uzee usio wa lazima naomba mchunguze watu wengi wamepata madhara baada ya kutumia dawa hizi.Utazifurahia kwa mda mfupi lakini madhara yake ni makubwa. 

Sunday, December 11, 2016

DALILI ZA NDOA ILIYOKUFA.

By On December 11, 2016
Kuna mambo mengi ambayo hupelekea ndoa kufa,leo nitazungumzia dalili chache zinazo onyesha ndoa kuelekea kufa.

Alichokipanga Mungu  mwanadamu si rahisi kupangua.


  1.  Wanandoa wanaposhindwa kutatua migogoro yao wenyewe. 
  2. Mwanandoa anapodhani anaweza kuishi mwenyewe bila mwenza wake.
  3. Wanandoa wanapoona kuwa watoto ndiyo sababu pekee inayowafanya kuendelea kuwa katika ndoa.
  4. Wanandoa wanapoanza kuogombana ndani ya ndoa,yaani kila mmoja anahofu kujadiliana na mwenzi wake masuala yanayo wahusu.
  5. Pale  mwanandoa unapogundua kuwa ndani ya ndoa kuna mambo mengi mabaya yanayofanyika kuliko mazuri.
  6. Wakati mwingine unaona mwenzi wako hakushirikishi masuala muhimu mpaka hatua ya mwisho unapogundua mwenyewe.
  7. Kugombana kwa suala moja kila wakati.
  8. Wakati mwingine mmoja wenu au wote mnapokosa hamu ya tendo la ndoa.
  9. Kupata uzito katika mawasiliano unapotaka kuwasiliana na mwenzi wako.Mume au Mke.
  10. Heshima aliyokuwa anakupa mke/mme mbele za watu inapopungua.Kama yote haya yatafanyika kinyume kwa kuyaweka katika hali yenye faida basi ndoa inaweza kudumu zaidi.Usisite kutoa maoni yako hapo chini kama umevutiwa na makala hii.

KWANINI MWANAMKE NI NGUZO KATIKA FAMILIA.

By On December 11, 2016
Kama nilivyokwisha eleza katika makala iliyopita kuhusu majukumu ambayo mwanamke anayo hapa duniani,Leo nitakupa sababu kwanini huyu mwanamke ni muhimu katika familia zetu na hata dunia kwa ujumla.
PICHA YA JIKONI.

Mwanamke ni mlezi wa mtoto.

Jambo lolote huanza katika hali ya udogo/uchanga hata mbuyu ulianza kama mchicha,lakini tukiangalia upande wa binadamu tunaona mwanamke jinsi ambavyo anapitia majukumu mengi katika kumlea mtoto aliye katika hali ya uchanga mpaka anapofikia umri wa kujitambua.

Watu maarufu wote na wale wasio maarufu wamepita katika mikono ya mwanamke,Kama mwanamke angeshindwa kumlea mtoto basi sijui nyakati hizi zingekuwaje bila wao.Hivyo ndiyo sababu wanawake wengi wanaupendo,wavumilivu katika mateso wanayopitia kutokana na malezi wanayopitia katika makuzi ya watoto.

Mwanamke ni mmiliki wa jiko.

Jiko ndiyo ofisi kuu ya mwanamke na mwanamke asiyeweza kupika bado hajakamilika kuwa mwanamke ni vema pia hata kuchua mafunzo ya kupika.Mwanaume jukumu lako wewe ni kutafuta kipato kwa ajili ya familia lakini mwanamke anaweza kufanya shughuli za maendeleo bila kusahau kuwa jiko bado ni sehemu yake muhimu,kumuandalia mume chakula kizuri,wote tunafahamu kuwa bila chakula hakuna jambo linaweza kwenda,mwili wa mwanadamu unategemea chakula ili kuweza kupambana na mihangaiko ya kila siku.

Siri unayopaswa kuifahamu mwanamke ni kuwa jiko ndiyo silaha yako hata pale unapogombana na mume wako jitahidi kumfurahisha anaporudi nyumbani mwandalie msosi mzuri anaopenda,tena ikiwezekana kile anachokipenda kifanyie ubunifu kionekane cha tofauti kwa mchele mmoja mapishi mbalimbali sio kila siku wali mweupe badilisha,unapobadili muonekano wa chakula unawavutia walaji.Vilevile muonekano wa vyombo vya chakula ni muhimu.Nimatumaini yangu umepata ujumbe kidogo.Usiache kutoa maoni yako hapo chini.

MAJUKUMU YA MWANAMKE DUNIANI

By On December 11, 2016
Wanawake duniani wanaonekana kama viumbe dhaifu wasioweza kusimama wenyewe katika kupambana na maisha.Ukitazama majukumu waliyopewa hayawezi kulingana na huo usemi hata siku moja.Mwanamke ana majukumu mengi kwanza ana miliki uzao,chimbuko na pia ni mtawala wa jiko.Ukiyaangalia maneno hayo matatu utaamini kuwa mwanamke anatawala ulimwengu.

Hata shetani anaufahamu ukweli kuwa akimwachia mwanamke apambane katika maendeleo na kumtafuta Mungu basi anaweza kutawala ulimwengu
.Kuna majukumu machache leo nitayataja aliyonayo mwanamke.

  1.  Mwanamke alipewa Neema ya kumzaa Yesu.luka1:26-35
  2. Wanawake walijitoa katika huduma ya Yesu.luka 8:2
  3. Mwanamke alimpaka Yesu mafuta kumuandaa kwa kifo chake.Yoh.12:3
  4. Wanawake walikuwepo msalabani.
  5. Wanawake walikuwa wa kwanza kumuona Yesu alipofufuka.Mathayo28:1-9 
  6. Wanawake wanajali na wanaupendo kuliko wanaume.
  7. Wanawake hujenga nyumba.Mithali 14:1
  8. Wanawake wanaweza kuomba kuliko wanaume.
  9. Mwanamke ni mzazi wa mwanaume
  10. Mwanamke ni mzazi wa kila kilichohai.
Baada ya kuona hayo majukumu machache nadhani wewe mwanamke au mwanaume unayesoma makala hii utaelewa thamani aliyonayo mwanamke.Mwanamke unapaswa kutambua hayo majukumu na kusimama vema kiroho pia katika kupambana na maisha usikubali kurudi nyuma hata kama unapitia magumu katika ndoa yako songa mbele,vumilia kwani wanawake tume pewa upendo na uvumilivu,Kumbuka pia kuwa sisi ndiyo waombaji wazuri na vilio vyetu vinafaida sana katika maombi tuendelee kuwa wanyenyekevu na kuziombea familia zetu.



3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu