PICHA YA JIKONI. |
Mwanamke ni mlezi wa mtoto.
Jambo lolote huanza katika hali ya udogo/uchanga hata mbuyu ulianza kama mchicha,lakini tukiangalia upande wa binadamu tunaona mwanamke jinsi ambavyo anapitia majukumu mengi katika kumlea mtoto aliye katika hali ya uchanga mpaka anapofikia umri wa kujitambua.Watu maarufu wote na wale wasio maarufu wamepita katika mikono ya mwanamke,Kama mwanamke angeshindwa kumlea mtoto basi sijui nyakati hizi zingekuwaje bila wao.Hivyo ndiyo sababu wanawake wengi wanaupendo,wavumilivu katika mateso wanayopitia kutokana na malezi wanayopitia katika makuzi ya watoto.
Mwanamke ni mmiliki wa jiko.
Jiko ndiyo ofisi kuu ya mwanamke na mwanamke asiyeweza kupika bado hajakamilika kuwa mwanamke ni vema pia hata kuchua mafunzo ya kupika.Mwanaume jukumu lako wewe ni kutafuta kipato kwa ajili ya familia lakini mwanamke anaweza kufanya shughuli za maendeleo bila kusahau kuwa jiko bado ni sehemu yake muhimu,kumuandalia mume chakula kizuri,wote tunafahamu kuwa bila chakula hakuna jambo linaweza kwenda,mwili wa mwanadamu unategemea chakula ili kuweza kupambana na mihangaiko ya kila siku.Siri unayopaswa kuifahamu mwanamke ni kuwa jiko ndiyo silaha yako hata pale unapogombana na mume wako jitahidi kumfurahisha anaporudi nyumbani mwandalie msosi mzuri anaopenda,tena ikiwezekana kile anachokipenda kifanyie ubunifu kionekane cha tofauti kwa mchele mmoja mapishi mbalimbali sio kila siku wali mweupe badilisha,unapobadili muonekano wa chakula unawavutia walaji.Vilevile muonekano wa vyombo vya chakula ni muhimu.Nimatumaini yangu umepata ujumbe kidogo.Usiache kutoa maoni yako hapo chini.
No comments:
Post a Comment