Katika
safu hii utaweza kufahamu na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu
urembo na mitindo ya mavazi kwa wanaume na wanawake, na hivyo kukufanya
msomaji kwenda na wakati na kuonekana wa kisasa zaidi.
Katika
makala hii ya mwanzo kupitia safu hii nitajikita katika kuzungumzia juu
ya uvaaji wa skafu pamoja na kukujuza mavazi yanaoendana na skafu.
Kwa
kuanza kabisa napenda utambue kuwa skafu ni kitambaa kinachovaliwa
shingoni kama urembo, unaweza kuvalia na aina yoyote ya nguo kwa
kuzingatia muktadha na vazi unalovalia.
Kuna
aina mbalimbali za skafu kutokana na aina ya kitambaa pia ukubwa na
muundo wa skafu, mfano kuna skafu ndefu, fupi na nyingine zamraba.
Skafu hizi zimetengenezwa kwa kutumia shanga mchanganyiko, ni rahisi sana unaweza kuzitengeneza hata unapo kuwa nyumbani. |
Katika
Miji mbalimbali yenye hali ya baridi, imekuwa kawaida sana kuwaona
vijana na watu wengi, wanawake na wanaume wakiwa wamevaa skafu kwani ni
moja ya vazi linalomfanya mtu aonekane nadhifu na kupendeza zaidi.
Kuna njia tofauti za kufunga skafu, na hii mara nyingi hutokana na aina ya nguo mtu aliyovaa pamoja na sehemu anayokwenda.
Unaweza
funga skafu kwa kulinganisha pembe zilingane na pia unaweza kufunga
katika nusu ya urefu, kisha kuiweka kwenye shingo yako ili mwisho moja
iwe ndefu nyingine iwe fupi kufanya fundo huru katika pande zote.
Zile
skafu ambazo zipo mraba unaweza kuikunja kwanza kama pembetatu kisha
kuiweka shingoni huku ukiifungia nyuma ya shingo na ukaonekana nadhifu.
Skafu
huvaliwa na wanaume na wanawake, ingawa mara nyingi wanawake ndiyo
wenye uwanja mpana sana wa kuvaa skafu. Skafu uweza kuvaliwa na nguo
yeyote pia husaidia kuongeza mvuto wa vazi ulilovaa.
Sehemu
za baridi mara nyingi utaona watu wakiwa wamevaa skafu ilikujikinga na
baridi na kipindi cha baridi ni vyema ukitumia skafu nzito na ufungaji
wake lazima uwe ule wa kuzungusha shingoni kama duara.
Licha
ya skafu kuvaliwa shingoni, pia inaweza kutumika kama kibanio cha
nywele na wengine wanazitumia kama mkanda, na pia unaweza kuifunga skafu
yako pembeni ya mkoba wako ikiwa ujapenda kuivaa shingoni lakini hapa
ni zile skafu fupi ambazo siyo ndefu ndiyo unaweza kuzifunga pembeni ya
mkoba wako.
Unashauriwa
ukivaa skafu usivae mkufu kwasababu hauwezi kuonekana na pia, ni vyema
kuvaa skafu nzito kipindi cha baridi na wakati wa jioni, mchana
unashauriwa kuvaa skafu ambazo ni nyepesi kulingana na hali yahewa
itakavyo kuwa.
Skafu asili ,unaweza kuzivaa shingoni katika muktadha wowote . |
Ukiwa umevaa vazi la Ofisini pendelea kuvaa skafu fupi kulingana na vazi ulilo vaa.
MWISHO…
No comments:
Post a Comment