Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, December 10, 2016

MAMBO AMBAYO HOUSE GIRL HUYAFAHAMU KULIKO MAMA MWENYE NYUMBA.

Wanawake wengi kwa asilimia kubwa huwaachia wadada wa ndani majukumu  ya nyumbani,hata wakati mwingine kazi wanazopaswa kufanya wao, dada wa ndani hufanya,Katika mtaa mmoja niliokuwa nikiishi kuna dada wa ndani ambaye alikuwa rafiki yangu,dada huyo alikuwa akinisimulia mambo mengi kuhusiana na mama mwenye nyumba.Jambo lililonishangaza ni mama mwenye nyumba kumpa dada wa ndani nguo zake za ndani pamoja na nguo za mmewe.Yule binti anasema "huwa nafua nguo za ndani za mama na baba",Hapa mwanamke ukiibiwa mume wako utamlaumu nani?.
Leo naomba nitaje mambo machache ambayo wadada wa ndani wanayafahamu katika usafi wa nyumba kuliko mama mwenye nyumba.

Kama house girl anatandika hivyo kitanda, wewe mwanamke mwenye nyumba ni kuamka na kuondoka, utaacha kuibiwa kweli


 Jinsi ya Kutumia Mkate.

Mkate ni kifungua kinywa ambacho hutumika na  watu wengi.Wat hupendelea kutumia mkate wakati wa asubuhi.Kuna siri kubwa sana nyuma ya mkate,naweza ukatumika katika kusafishia picha za ukutani na kava{cover} la kitabu.Hakikisha  unaloweka kidogo ili usiwe mkavu sana au nyunyuzia maji kwa mbali lakini kwa mikate milaini unaweza safishia bila kuuloweka.




Jinsi ya kusafisha  Chupa ya chai{Thermos}.

Tumia maganda ya mayai{kaka ya yai} baada ya kuyapasua kisha weka ndani ya chupa changanya na vinegar au Limao acha kwa masaa kadha au lisaa limoja kisha tikisa kama uoshavyo chupa.baada ya hapo osha vizur kwa maji safi na sabuni na kuikasha.


Usafishaji wa kabati.

   
Ni vema kusafisha  kwa kutumia dawa kabati  lako la nguo pamoja na droo,sehemu unayoweka nguo hata mara moja au mbili kwa mwaka.Hii itasaidia kuzuia wadudu kama mende kutozaliana na kutaga mayai katika kabati lako.kisha panga kabati lako katika mpangilio mzuri.kama nichupi au boksa,suruali,magauni jua sehemu ya kuziweka ili wakati wa kutafuta nguo ya kuvaa usivurugue kabati zima nakuliacha katika muonekano mbaya.



Jinsi ya kuondoa uchafu bafuni hata katika masink.

Tumia kikombe kimoja cha limao{vinegar} kisha changanya na vikombe vitatu vya maji,baada ya hapo anza kusafishia masink yako  vizuri.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu