Enter your keyword

Culture for Life.

Tuesday, February 26, 2013

False eyeleshes(Namna ya kutumia kope bandia)

By On February 26, 2013


kope bandia

jicho ambalo lisha valishwa kope bandia

Gundi ya kope bandia
Watu wengi hupenda kope ndefu na kulazimika kutumia kope bandia hasa wenye kope fupi na wale wenye macho madogo,Unapotumia kope bandia hufanya macho yako yaonekane vizuri na yavutie zaidi.Vitu utavyohitaji kabla ya kuweka kope bandia ni :Kope bandia zenyewe, gundi ya kope bandia(False eyelash glue)Maskara na kioo.Njia ambazo zitakusaidia wakati wa kuweka kope bandia hasa  ambao hawapendi kwenda saluni na wana uwezo wa kuweka wenyewe.

1.Chagua kipimo sahihi cha kope bandia.kabla ya kuweka Gundi katika kope hakikishaumechagua urefu sahihi wa kope unazohitaji,pia acha Gundi ikauke kwanza kidogo kisha bandika kope zako,acha iendelee kukauka yenyewe pia usiishikilie wala kukandamiza ili kope zishike vizuri usifanye hivyo ukimaliza kubandika achia na zitaendelea kukauka zenyewe.
    
2.Tumia maskara (mascara)  kwenye kope bandia,ukipaka maskara kwenye kope zako zitazifanya zionekane asilia,unaweza kutumia maskara rangi nyeusi na blauni.


3.Tumia wanja wa maji,unaweza kuupaka kwenye mstari wa kope ya juu ili kuficha uwazi uliopo baada ya kuweka kope bandia  pia unaweza kutumia wanja mweusi au blauni kulingana na na ngozi yako na wanja unaopendelea kuutumia.

4.Tumia kitu cha maji maji(makeup remover)ambacho husadia kuondoa kope bandia kwa urahisi zaidi,baada ya hapo unaweza kutoa taratibu kope zako.

Zingatia:
Hakikisha unazisafisha vizuri hizo kope na kuziweka mahali salamakama unampango wa kuzitumia tena.
Tumia kitu cha maji maji kuzisafisha(makeup remover)ili kuweza kuondoa maskara pamoja na wanja 
Hakikisha unaondoa kope bandia kabla ya kwenda kulala
Usipende kuchangia kope bandia na mtu yeyote wala vipodozi vya usoni ilikuepuka maambukizi yasiyo na tija
Endapo gundi itaingia kwenye macho hakikisha unaosha haraka na maji ya moto kiasi au uvuguvugu.
Pia ni muhimu kuosha mikono yako kabla hujaanza kuweka kopebandia

Mwisho kabisa mpenzi msomaji wa safu hii hakikisha unatumia kope hizi za bandia vema nikiwa na maana kwamba kuna kope zingine ni za rangi.Itakuwa ajabu mtu atakapo tumia kope za rangi wakati anaelekea kanisani,sababu utafanya watu wote wawe wana kutazama wewe,tumia kope bandia lakini zingatia mandhari unayokwenda.Usisite kunitumia maoni kupitia namba yangu ya simu kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno au barua pepe.
abnerytupokigwe@gmail.com ,   0756 377940
      

   

Monday, February 18, 2013

MAZISHI YA Askofu Thomas Laizer

By On February 18, 2013
Familia ya marehemu ikiwa katika picha ya pamoja kwenye kaburi la marehemu muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kupumzishwa katika kaburi lake.

Rais Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Askofu Dk.Thoma Laizer

Maaskofu na wachungaji kutoka dayosisi mbalimbali za KKKT wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer, alhamis iliyopita siku moja  kabla ya mwili huo kuzikwa

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Marais wastaafu Benjamin Mkapa, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa, wakifuatilia ibada ya mazishi ya Askofu Thomas Laizer ijumaa iliyopita.

Saturday, February 16, 2013

Emerald green rangi ya mwaka 2013

By On February 16, 2013


 KIJANI

Kampuni ya Pantone ya Marekani ambao ni wataalamu wa kuangalia rangi iliyoshika chati katika masuala ya mitindo kila mwaka, wameichagua rangi ya kijani kuwa rangi ya mwaka 2013, baada ya kupiga kura  na kufanya utafiti wa rangi ya mwaka huu  kupitia Wanamitindo mbalimbali.Kwaheri rangi ya Zambarau (purple color) ambayo ilishika chati mwaka jana katika mitindo mbalimbali na hata katika Sherehe za Harusi.

Ni wazi kuwa rangi hii huwa tunaiona mara kwa mara. Ni rangi  yenye kutia moyo na neema.

Hakuna rangi yenye kuonyesha ufufuo zaidi ya kijani ni kiwa na maana ya kuwa rangi hii hutupa matumaini siku zote, mfano halisi ni katika mazao yetu.


Njia tano ambazo zitatuunganisha na rangi hii ya kijani katika maisha yetu ya kila siku.

Chakula:    Ni wazi kuwa ni lazima tule mboga za majani, matunda pamoja na juisi katika kila mlo wetu, mwaka huu wa 2013.Watanzania tulio wengi hupendelea kula mboga za majani isipo kuwa upande wa matunda bado hali ni tete kwa baadhi ya wananchi.Watu husema familia bora ndiyo hukamilisha mlo kamili.Mpenzi msomaji kama huwezi kuvaa nguo ya kijani basi iwakilishe rangi hii kupitia chakula chako.

Nguo: Unaweza kuvaa jeans ya kijani na kuoanisha na vikorombwezo vyako vya rangi ya mchanga (beige) gold, na blauzi nyeupe (white top),pia vaa gauni la kijani na mkanda mwekundu, rangi hizi zinakwenda pamoja na utapendeza sana.Upande wa wanaume ukivaa tisheti la kijani,nyeusi au nyeupe una weza kuvalia na jeans rangi yoyote bila kusahau chini kuvaa raba zenye rangi nyeupe ambayo itakuwa na  rangi zingine kwa mbali na kijani ikiwepo au unaweza kuvaa raba ya kijani kabisa ila hakikisha juu umetupia tisheti au shati la mikono mifupi ambalo rangi kuu iwe nyeupe.

Matembezi: jitahidi kutembelea sehemu tulivu mwaka huu 2013,sehemu zenye bustani nzuri nikimaanisha mandhari ya kijani haswa,naamini itakuvutia sana na utakuwa umeiwakilisha vema rangi ya kijani pia usisahau kupanda maua, miti pamoja na  kuwa na bustani yako ya mboga za majani na miti ya kivuli na matunda  katika nyumba yako hata kama huna eneo jaribu hata kupanda katika ndoo,kuna mboga kama mchicha ambazo kuweza kumea katika chombo kidogo kama ndoo au vyungu vya maua.

Michoro:Unaweza kuiwakilisha rangi hii kupitia michoro,weka michoro yenye picha zenye rangi ya kijani katika ukuta wako mfano maua,picha za watu,pia unaweza kutumia maua yenye rangi ya kijani ambayo hubandikwa ukutani.Hakika utafurahia mandhari ya nyumba yako na pia itakusaidia kuondoa mawazo unapokuwa umechoka.Mpenzi msomaji endelea kuungana nami katika safu hii,

Wednesday, February 13, 2013

color of the year 2013

By On February 13, 2013
pic by,weddingbellstz.blogspot.com




Tuesday, February 12, 2013

Ndoa za Arusha: Harusi, Virusi, Kiharusi

By On February 12, 2013

 Na Mpanda Vifodi


 Sasa ni katika moja ya hizo safari za kwenda Uswahilini ambapo lilizuka gumzo linalohusu ‘Ndoa za Arusha,’ ‘Wanandoa,’ na ‘Maovu yanayofanywa na wanandoa wenyewe hapa mjini …. Hapana sijazungumzia lolote kuhusu ‘Katerero!’ kwanza sijui maana yake ni nini.
 “Usitishwe na Ving’ora au Tarumbeta za Arusi, ndoa nyingi za Arusha huvunjika ndani ya mwaka mmoja tu tokea zifungwe.” Alisema msafiri mmoja ambaye sikupata fursa ya kumhoji kama yeye binafsi ameoa na ikiwa ni hivyo ndoa yake imedumu kwa muda gani.

 “Tena usitishwe kabisa na misururu mirefu ya magari siku za arusi, wala sare za wapambe, au pilau, ndafu, ‘Shampeini,’ na vile vinywaji ambavyo huwa vinasubiri hadi mchungaji na mwinjilisti waondoke ndipo vianze kusambazwa mezani.
 Na usijali kuwa wakati ndoa hiyo inafungwa Bibi Arusi tayari ni mjamzito na hakuna kithibitisho kuwa huyo ‘boya,’ anayemuoa ndiye mwenye hiyo mimba. Na usipate shida kujiuliza ikiwa Bwana Arusi naye anakumbuka hata jina la mkewe huyo mtarajiwa.

Na isikupe shida kabisa ikiwa utaona kama vile ‘Bwana Arusi,’ yuko bize akimfinyia jicho yule binti aliyeketi kiti cha Mbele kanisani na mbaye anatabasamu na kumtumia ujumbe wa simu unaosema; “Sweetie, nitakumiss leo jamani, lakini najua kesho tutakuwa wote, halafu Ahsante kwa ile M-Pesa ya jana, ila bado nahitaji Laki moja kwa ajili ya kodi ya Nyumba!”
 Hadi hapo sijaongea lolote kuhusu ‘Katerero,’ na hii ni kwa sababu sijui asilani hili neno huwa lina maana gani nyingine zaidi ya lile Gulio au Soko la akina Kiiza, tulilokuwa tunalisoma kwenye kile kitabu cha ‘Tujifunze Lugha Yetu (4).’
 Hivi tulikuwa tunazungumzia nini? Ooh! Ni kuhusu vifodi vya ‘Kidemi,’ Uswahilini,’ na mazungumzo ya wasafiri wake kuhusu jinsi ndoa za maharusi wa Arusha zinavyozungumza kabla hata ya ‘Kifo kuwatenganisha!’ hao waungwana.

Na tafadhali sana naomba usiendelee kulitaja hilo neno la ‘Katerero,’ maana kwanza halina uhusiano wowote na kile tunachokizungumzia hapa; isitoshe sijui hata vile vitabu vya zamani vya ‘Kiswahili,’ kwa shule za msingi vilipotelea wapi.Ila kwa wale wasiofahamu ni kwamba ‘Gulio,’ kama lile la kule ‘Katerero,’ ni soko la msimu au kwa lugha nyepesi, ‘Mnada!’ kama ule wa Ngaramtoni, Kisongo na Tengeru ambako watu hukusanyika ili kuuza na kununua na pia kuiba na kuibiwa bidhaa zao.

Na tunapozungumzia ‘Kuiba,’ na ‘Kuibiwa,’ watu hapa Arusha pia huiba wake au waume zao na wao pia kuibiwa wake au waume zao; ‘Ngoma droo!’ kama ambavyo wale ‘Machalii,’ wanaovaa ‘Njuti,’ kule Unga-Limited wanavyosema.Na maisha ya Arusha ni kama mnada; inadaiwa kunapokucha tu, watu wakielekea sehemu zao za kazi, biashara au uzururaji, mnada wa binadamu hufanyika. Naam zile dhambi zilizoshindikana huwa zinafanyika maofisini, viwandani, masokoni na hata mashuleni, na hasa kwenye vile vyuo vya ‘Maimuna,’ vinavyofundisha ‘English Course!’

Jioni kila mtu hurejea nyumbani, kwa mkewe au mumewe wakiwa wameshachoka na ‘Kazi,’ za mchana huku wakiwapigia kelele watumishi wa ndani au ‘Hausigeli,’ waharakishe kuleta chakula ili walale zao mapema.Siku hizi hakuna mtu anayelalamika kwenda kazini, maana sehemu za kazi zimegeuka kuwa

‘Magulio,’ naam kama yake ya Katerero, isipokuwa haya ya makazini hufanyika kila siku hayasubiri ule mnada wa Jumamosi Tengeru, Jumapili Ngaramtoni au Jumatatu Mbauda.Sasa hata kama minada hii ya siku za kazi hapa Arusha huwa haifanyiki kule ‘Katerero,’ kama ule wa ‘Kiiza,’ inadaiwa kuwa kuna kitu kinachoitwa ‘Katerero,’ katika hii minada na hii inachangia kuvunjika kwa ndoa nyingi hapa mjini.

 Na wakati mwingine hizi gulio za katerero za mjini hapa husababisha wababa wengine kurejea kutoka‘Safari za mbali,’ wakiwa ‘Wamevimba yote mapaja na kutetemeka mwili! Ugonjwa gani tena, Arusi, Kiharusi au Kirusi?Na kwa wamama na wadada kabla ya kutumbukia humo nao huwa wanapewa mistari kama ule wa lile shairi la ‘Kama mnataka mali ………!”
 chanzo cha story soma Gazeti la KUTOKA ARUSHA TOLEO LA 33,au tembelea website yetu www.kutokaarusha.com.

Saturday, February 9, 2013

What To Wear: Valentine's Day

By On February 09, 2013

white suit and red tie and red






pink shirt for men


night dress (all pic by google)




Vazi la siku ya wapendanao
Siku ya wapendanao ni siku ya kila mtu kuonyesha shukrani zetu kwa watu tunaowapenda na walio karibu na maisha yetu kwa njia moja au nyingine.Watu hao wanaweza kuwa mama,baba,dada,kaka,mpenzi,mchumba,mke,mume,ndugu,marafiki,wafanyakazi wenzako  pamoja na majirani .Kwa nini?  watu wengi huifanya siku hii maalumu  kila mwaka na kuangaika kutafuta nguo ya kuvaa siku hiyo na kuchagua rangi nyekundu pamoja na zawadi.

Mpenzi msomaji wa safu hii napenda ujue kuwa wiki hii ni wiki ya kuonyesha upendo na kuwa karibu zaidi na watu tunao wapenda  pamoja na kuwakumbuka hata ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki.Nimeona vema tukikumbushana baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia hasa katika suala zima la uvaaji.Zifuatazo ni njia ambazo zitakusaidia kufanikisha siku hii ya wapendanao.

Chagua rangi sahihi ya nguo
Njia ya kwanza iliyo rahisi na itakayo kufanya upendeze siku  hii ya wapendanao ni kuepuka kuvaa vitu vingi vyenye rangi nyekundu.Sio lazima kila mtu avae nguo yenye rangi nyekundu kama tulivyozoea.Rangi hii nyekundu ni vema ukiitumia kama kikorombwezo(Accesories)  katika mavazi yako,hakikisha huchanganyi rangi vibaya kwasababu mtu mwingine anaweza akavaa kijani na nyekundu na kumfanya aonekane kama mti wa krismasi.

Hakuna kitu kibaya kama kupendeza kupita kiasi mpaka unaharibu muonekano wako.Vaa kawaida na utavutia sana, ikiwa una  mtoko hahikisha unavaa kawaida mfano unakwenda  pikiniki, sinema au kupata chakula cha mchana,jioni na marafiki zako.Wanawake wanaweza  kuvaa jinsi au suruali ya kawaida,gauni na blauzi(top)yenye rangi ya krimu,nyekundu au pinki,Upande wa wanaume wanaweza kuvaa jinsi au suruali ya kitambaa kulingana na mazingira anayo kwenda na shati au tisheti rangi ya pinki,nyekundu au krimu.

Ifanye siku hii ya upendo

Endapo wewe na na mpenzi wako mnataka kuifanya siku hii kuwa ya furaha(romantic date) kwenu na mmepanga kwenda sehemu tulivu mnayoipenda au katika kumbi za starehe(club) ni vema ukivaa vizuri huku  ukihakikisha vazi utakalo vaa linakupa uhuru katika mtoko wako.Jaribu kuvaa gauni jeusi na mkanda mwekundu,oanisha na heleni zenye rangi nyekundu na kiatu cheusi au pia waweza kuvaa gauni nyeupe na skafu nyenye rangi ya pinki bila kusahau kuonanisha na heleni,bangili,mkufu,pochi,viatu kwa kuzichanganya rangi hizi tatu ambazo ni  pinki,nyekundu,na krimu.Jitahidi kutumia rangi mbili vizuri ili isiwe kachumbari sana.

Pia unaweza kuvaa pinki na rangi nyekundu rangi hizi pia huenda pamoja.Wanaume wanopenda kuvutia na kuwavutia wenzi wao siku hii ya wapendanao ni vema wakichanganya vema rangi hizo tatu katika mavazi yao mfano unaweza kuweka kitambaa chekundu katika mfuko wa shati au koti la suti ulilovaa au kwa wale wanao vaa saspenda wana weza kutumia  mikanda yenye rangi nyekundu ilikuongeza nakshi, vilevile sio mbaya kama ukivaa soksi nyekundu ni wazi kuwa haziwezi kuonekana,au tai nyekundu kwa wale wanao vaa tai.Wanaume ni vema mkizingatia mazingira ya mtoko wenu bila kusahau kuangalia mwezi wako kavaaje? ilimsipishane sana.Mbali na hayo unaweza kuvaa vazi ambalo mwenzi wako siku zote hupenda wewe uvae ila usihau kuchanganya japo moja ya rangi hizi tatu pinki,nyekundu na krimu.

Panga chumba chako
Samahani hapa naomba tukumbushane  kidogo kuwa siku hii  ni siku ya tofauti.Jaribu kukibadilisha chumba chako na kukipa muonekano wa tofauti kwa mwenzi wako jitahidi kuwa mbunifu kwa kuweka nakshi mbalimbali ili kukifanya chumba chako kuwa katika hali ya upendo zaidi (romantic place)siwezi kuzungumzia sana ila unajua nini cha kufanya kwa mwezi wako.Tukumbuke kuwa sivema vazi la kulalia liwe pajama au gauni jepesi refu/fupi  kama tulivyozoea jaribu kuvaa kitu cha tofauti kwaajili ya siku hii ni kiwa na maana kuwa unaweza kuvaa kitu cha tofauti ambacho kila mmoja wenu ajazoeleka na mwenzi wake kuvaa.




 






Thursday, February 7, 2013

Uzuri ni Maisha

By On February 07, 2013

Kuna kitu ambacho kinawagusa vijana na wazee kwa mpigo. Kitu hicho ni Uzuri. Muonekano wa mtu wakati fulani unaweza kukita uzuri kwenye upendo kwani jinsi mtu anavyofanana huchukua sehemu kubwa na muhimu katika suala la uchaguzi wa mwenza. Hivyo msemo wa , “Uzuri upo katika jicho la mtazamaji”. Ina maana kuna kitu kinachonekana. Magerezani siku hizi hupenyezwa vioo kwa lengo moja tu, kujiangalia wenyewe. Iwe mwanamme au mwanamke, kujiona / kujihisi umependeza ni tamanio la kila binadamu.
Hivyo ninawakaribisha kwenye safari hii ambayo tutaweza kuchunguza vipengele mbalimbali vinavyohusiana na urembo, moja hadi lingine. Kama mnavyoona, uzuri wa ndani ni muhimu sana katika maisha, lakini huwa hatuuoni kwa kutazama kwa haraka au kwa mara moja. Sisi huona uzuri unaonekana kwa upande wa nje (umbile) ambao pia ni muhimu. Kama ilivyo kwa wachungaji na washauri wengine pamoja na walimu wa kiroho tunataka kutafuta ufumbuzi wa uzuri wa nje ili kujenga uwiano na ndio sababu tunasema Uzuri ni Maisha.


Uzuri ni nini …. Ni sifa ya kupendeza jicho. Sasa nywele zako zinaweza kupendeza na uso wako pia, kucha zako zinaweza kupendeza, miguu yako hali kadhalika na hadi ngozi yako pia inaweza kupendeza. Na hivi ni vile vinavyoweza kuonekana na mtu yeyote. Sasa je, ni jinsi gani wewe unaweza kuja kujiona u mzuri? Ni nini hasa kinachotakiwa kutoka kwako hadi ufikie ile hali ya kuonekana mzuri na kumvutia mtazamaji? Ni nini hasa cha kutoka kwako hata juu yako kufikia hatua ya kusema, “Naaamm, mimi ni mzuri”? Hadi wewe mwenyewe unajiona umependeza, basi ni dhahiri unajisikia vizuri. Lakini je wewe huamka tu asubuhi na kujiona umependeza? Je wakati unapotembea ni ghafla unabadilika na kuanza kupendeza? Sidhani kama ni hivyo. Kuna mtu ambae amesababisha kupendeza kwako. Lazima utakua umeenda mahali ambako wanahusika na masuala ya kupendezesha sio? Kwa sababu huwezi kwenda hospitali na kutoka na kucha zilizopakwa rangi vizuri. Hutoingia ndani ya duka kubwa lolote na kutoka na nywele laini zilizooshwa na kunyooshwa. Hali kadhalika huwezi kufanya vitu hivi jikoni kwako. Kwa vitu hivi unakwenda sehemu maalum iitwayo SALUNI
 

Sasa basi, Saluni ni nini? Kwa ujumla ni mahali ambapo wanawake na wanaume wanakwenda kupata huduma ya zinazohusiana na mitindo ya uzuri wa nywele, kucha na mwili mzima wakati wametulia. Hii inaashiria kwamba watu ambao utawakuta sehemu hiyo watakua na uwezo na watakua na muda wa kukufanya utulie na ujisikie uko nyumbani ingawa sehemu yenyewe sio nyumbani kwako. Watu hawa ni wa muhimu sana katika masuala ya uzuri. Sasa kabla ya kuzungumzia huduma utakazozipata hadi kufikia kupendeza kwako, tuangalie kwanza ni nani ambae tutataka akupatie huduma. Ni akina nani hawa, hivyo matarajio ni nini? Je wana sifa za aina gani kabla hujawakabidhi hazina yako yenye thamani sana. Ndio, kitu chochote kinachohusiana na uzuri wako ni hazina yako.
 Kitu cha kwanza na cha muhimu mtoa huduma awe na elimu juu ya kile atakachokufanyia. Lazima awe na uzoefu na huduma hiyo. Hii ni muhimu iwapo lengo la kupendeza linataka kufikiwa. Usiridhike na kufurahia huduma ambayo kesho yake itakugharimu na kukuletea majuto. Hakikisha mtu atakayekuhudumia ana uzoefu na ujuzi wa kile atakachokufanyia
 

 Ushauri – mtoa huduma lazima awe na uwezo wa kukuuliza taarifa zinazohusiana na matibabu ya awali ambayo ulishayapata. Hii ni muhimu kwa sababu kuna matibabu mengine ambayo yakichanganywa na ya aina nyingine yanaweza kusababisha sumu. Hivyo ni haki yako kuwa na wasiwasi na mtoa huduma ambae hatakudadisi kuhusu historia yako na badala yake ataendelea kutoa ushauri unaohusiana na vitu vya kufanya au ambavyo usifanye kuhusiana na tiba ulizozipata awali
 Mtoa huduma mzuri ataweza kuelezea wazi na kukuelewesha kikamilifu mtiritiko mzima utakaohusiana na mchakato wa kukupendezesha na kwamba sio
mazingaombwe. Maneno mazuri ni sawasawa na kuchua roho. Iwapo kila kitu kinawasilishwa sawasawa unaweza kutulia na kufurahia huduma zenyewe. Iwapo mtoa huduma atajieleza vizuri, kazi inakua rahisi zaidi na wateja wote wataweza kuhudumiwa kwa usawa.
 

 Mtoa huduma awe mfano mzuri wa usafi utakaojumuisha kucha zilizokatwa vizuri, mkono misafi ambayo haining’inii mapambo ya vito, awe na mavazi ya kujisitiri, na avutie makundi yote ya watu.
 

 Kipimo kikuu cha mtoa huduma mzuri ni uwezo wa kufanya kazi yake kwa makini bila ya kumfikiria mteja aliyeondoka au ambae atakuja. Lazima akoleze na alenge mawazo na juhudi yake kwa mteja aliopo wakati ule. Maisha yake ya binafsi yasiingiliane na kazi yake. Unapokwenda salon unaweza kupumzika na kuongelea maisha yako lakini hii haimpi nafasi mtoa huduma ya kuanza kukuelezea shida zake. Ni wajibu wake (mtoa huduma) kukusaidia au kukufariji au kukufurahia lakini hali hii haimpi mtoa huduma haki ya kuyasambaza mazungumzo hayo. Siri za mteja lazima ziheshimiwe wakati wote bila kujali wao ni nani.
 

 Ifuatayo inaweza kuleta mabishano lakini ni ukweli ambao usemwe. Mtoa huduma mzuri hatokuruhusu umuamrishe nini, lini, kipi na vipi kuhusiana na vitu atakavyotumia kwenye tiba yako. Yeye ndio mtaalam hivyo ni yeye wa kukueleza na kukushauri kutokana na mahitaji yako. Usihatarishe uzuri wako kwa kubahatisha. Kwa vile vitu fulani vimemsaidia mteja fulani haimaanishi ya kwamba vitakusaidia na wewe pia.
 

 Utaujua ukweli na ni ukweli huo ndio utakuweka huru. Mtoa huduma mzuri atakueleza ukweli hata kama ukweli huo utakuongoza kwenye kutokufanya huduma ambayo wewe unaitaka. Hii inadhihirisha ya kwamba mtoa huduma mzuri halengi kwenye utengenezaji pesa peke yake bali pia anafikiria hatima yako kutokana na maamuzi ya haraka na mepesi unayotaka kuyafanya. Ni lazima akueleze faida na hasara za huduma husika.
Kwa kifupi sasa unawaelewa watu ambao utawakuta ndani ya salon na hivyo unaweza kuwa na mategemeo kwamba utaridhika na huduma utakazopata. Uelewa huu utakusaidia kufanya maamuzi iwapo unataka kuwa mteja (client) au mshitiri (customer). Kila wakati jiangalie iwapo wewe ni mteja au mshitiri.
Mteja ni yule anayekwenda kwa mtaalam kwa madhumuni ya kupata ushauri wa kitaalam na hatimaye kuajiri huduma za huyo mtaalam. Mteja haruki kutoka mlango mmoja hadi mwingine. Mteja ana umiliki wa sehemu

Mshitiri ni mtu anayetafuta huduma ya aina fulani bila kujali atakapoipata. Yeye anachokitaka ni huduma. Mshitiri hana umiliki wa sehemu

Imetayarishwa na Russell Davies Touch

Beauty is Life

By On February 07, 2013


There is one thing which affects the young and the old alike. Its one's beauty.How one looks at a given time.you can link beauty to love as looks plays an important role in the choice of a mate. Thus they say beauty lies in the eyes of the beholder. It means there is something to be seen.In prisons nowadays they smuggle in mirrors for only one purpose,to see themseves.It be men or women,looking good is the desire of every human being.

I therfore welcome you to this journey of which we will be exxploring different aspects of beauty,one by one.You see,inner beauty is very essential in life,but its not what we see by a quick look look.we see your outerward beauty.it means its also important.Just as Pastors and mentors and other spiritual taechers seek to address our inner beauty,we will seek to address the outer beauty to create a balance.thats why we say Beauty Is Life.

What is beauty,its simply a quality thats pleasing to the eye. Now.your hair can be pleasing.your face can be pleasing,your nails can be pleasing,your feet can be pleasing and your skin can be pleasing. This is what anyone can see.Now how do u come to be seen beautiful? What does it take for you to reach the state of looking good and pleasing to the on looker.? What does it take for you even onyourself to say yeeees im looking beautiful? When you are looking pleasant,then definately you feel good.But then,do u just wake up in the morning looking good? Do you all of a sudden while walking just transform and start looking good? I guess not. Someone is responsible for your looking good.you mus have gone to a place where they deal with the subject of looking good,right? Because you wont go inthe hospital and come out wth nicely painted nails. You wont enter the supermarket and come out with silky hair washed and relaxed. Its not something you can get done in your kitchen. You go to a place called a salon.

What is a salon? Its generally a place where women and men go to relax while their hair and nails and body is attended to. it therefore implies that the people you are going to meet at the salon must be able and be prepared to make you relax and feel at home though it wont be your home.these are the most important people as far as attaining beauty is concerned.Now before we talk about the services you can get in the salon to beautify yourself,lets first of all examine who is it from whom we must demand service.Who are they exactly,and what must be our expectations? What qualities must they possess before you trust them with your most valuable treasure.yes anything which  part of your beauty is your treasure.

*The first and crucial thing is the service provider must be educated as to what they are going to do.They must have relevant experience.this is very important if pleasing results have to be achieved.Dont just be happy to receive today a service which tomorrow will cost you and you regret.Make sure the person attending to you has experience and possess knowledge of what they are about to do

*Consultation- the service provider must be able to ask the historical information about the previous treatments you had.this is very essential since some other treatments are poisonous to each other.Its your right to have doubts if the service provider doesnt care about your history and to give advice as to what you can or may not do in relation to your previous treatments

*A good service provider will be able to talk clearly and make you understand whats going on.your beautification process is not magical so it can be communicated clearly.Good words are like massage to the soul.when everything is communicated properly you can relax and enjoy the services.If the service provide can talk clearly it also makes work easier and all clients treated equally.

*A good service provide must be the enforcer of cleanliness,well trimmed nails,clean hands and free from dangling jewelery.dress modestly,to appeal to all groups of people.

*Concerntration must be the mark of a good service provider.They mus not worry about the previous client.and must not think of the next client.they must put all their effort on the client at hand.Personal life of the service provider must not interfere with work..When you go to a salon,yes u might relax and talk of your life,that does not give the service provider to open to u their problems also.they should help you or comfort you or rejoice wth you but not to spread it around.The privacy of the client must be respected at all times irregardless of who they are.

*this one is a little bit controversial but thats the truth and we will say it. A good service provider will not allow you to dictate to them what,when,which and how,of the treatments to use.They are the experts soo they are the ones to tell you and advise you according to your needs.Dont risky your beauty with guess work service providers.Just because something worked for so and so doesnt guarantee that it will work for you too.

*You shall know the truth and the truth shall make you free.A good service provider will tell you the truth even if it might lead to you not doing a particular service you wanted to.it implies that a good service provider must not only focus on making money out of you but also must take into consideration what will happen to you if one take short cuts.You mus be told of the advantages and disadvantages of particular services


in Short now you understand what the people you have to meet at the salon must at least possess.you now know a bit of what to expect.if the service provider provide their services to satisfication.it will then make u decide whether you want to be a client or a customer.Always check yourself if you are a customer or a client،

A client is someone who goes to a professional to look for professional advice and engage the services of that professional.A client does not hop from door to door.A client belongs to

A customer is somone who is looking for a particular service and does not mind where they get it.all what they are after is that service.Customers dont belong to

Monday, February 4, 2013

MAZENGO TRADERS

By On February 04, 2013

Mazengo Traders Arusha.IF YOUR AWAY FROM ARUSHA

PLEASE CONTACTS US THEN WE WILL ORGANIZE HOW TO DELIVER

  +255 756 377 940



ARUSHA HAND CRAFTS,TV STAND DESIGNER BY Mazengo Traders




Add caption

Msikiti SOFA DESIGNER Mazengo TRADERS


TV STAND DESIGNER MAZENGO TRADERS

SUN BED COACH DESIGNER MAZENGO TRADERS


SUNBED COACH DESIGNER MAZENGO TRADERS ARUSHA

SITTING ROOM AND DINING DESIGNER MAZENGO TRADERS ARUSHA



SUNBED COACH DESIGNER MAZENGO TRADERS ARUSHA

MSIKITI COACH DESINER MAZENGO TRADERS ARUSHA


SITTING ROOM DESIGNER MAZENGO TRADERS ARUSHA



MCHANUKO COACH DESIGNER MAZENGO TRADERS ARUSHA




CUPBOARD DESGNER MAZENGO TRADERS ARUSHA

SUNBED COACH AND POFU STOOL DESIGNER MAZENGO TRADERS ARUSHA




BED DESIGNER MAZENGO TRADERS ARUSHA



3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu