KIJANI
Kampuni ya Pantone ya Marekani ambao ni wataalamu wa kuangalia rangi iliyoshika chati katika masuala ya mitindo kila mwaka, wameichagua rangi ya kijani kuwa rangi ya mwaka 2013, baada ya kupiga kura na kufanya utafiti wa rangi ya mwaka huu kupitia Wanamitindo mbalimbali.Kwaheri rangi ya Zambarau (purple color) ambayo ilishika chati mwaka jana katika mitindo mbalimbali na hata katika Sherehe za Harusi.Ni wazi kuwa rangi hii huwa tunaiona mara kwa mara. Ni rangi yenye kutia moyo na neema.
Hakuna rangi yenye kuonyesha ufufuo zaidi ya kijani ni kiwa na maana ya kuwa rangi hii hutupa matumaini siku zote, mfano halisi ni katika mazao yetu.
Njia tano ambazo zitatuunganisha na rangi hii ya kijani katika maisha yetu ya kila siku.
Chakula: Ni wazi kuwa ni lazima tule mboga za majani, matunda pamoja na juisi katika kila mlo wetu, mwaka huu wa 2013.Watanzania tulio wengi hupendelea kula mboga za majani isipo kuwa upande wa matunda bado hali ni tete kwa baadhi ya wananchi.Watu husema familia bora ndiyo hukamilisha mlo kamili.Mpenzi msomaji kama huwezi kuvaa nguo ya kijani basi iwakilishe rangi hii kupitia chakula chako.
Nguo: Unaweza kuvaa jeans ya kijani na kuoanisha na vikorombwezo vyako vya rangi ya mchanga (beige) gold, na blauzi nyeupe (white top),pia vaa gauni la kijani na mkanda mwekundu, rangi hizi zinakwenda pamoja na utapendeza sana.Upande wa wanaume ukivaa tisheti la kijani,nyeusi au nyeupe una weza kuvalia na jeans rangi yoyote bila kusahau chini kuvaa raba zenye rangi nyeupe ambayo itakuwa na rangi zingine kwa mbali na kijani ikiwepo au unaweza kuvaa raba ya kijani kabisa ila hakikisha juu umetupia tisheti au shati la mikono mifupi ambalo rangi kuu iwe nyeupe.
Matembezi: jitahidi kutembelea sehemu tulivu mwaka huu 2013,sehemu zenye bustani nzuri nikimaanisha mandhari ya kijani haswa,naamini itakuvutia sana na utakuwa umeiwakilisha vema rangi ya kijani pia usisahau kupanda maua, miti pamoja na kuwa na bustani yako ya mboga za majani na miti ya kivuli na matunda katika nyumba yako hata kama huna eneo jaribu hata kupanda katika ndoo,kuna mboga kama mchicha ambazo kuweza kumea katika chombo kidogo kama ndoo au vyungu vya maua.
Michoro:Unaweza kuiwakilisha rangi hii kupitia michoro,weka michoro yenye picha zenye rangi ya kijani katika ukuta wako mfano maua,picha za watu,pia unaweza kutumia maua yenye rangi ya kijani ambayo hubandikwa ukutani.Hakika utafurahia mandhari ya nyumba yako na pia itakusaidia kuondoa mawazo unapokuwa umechoka.Mpenzi msomaji endelea kuungana nami katika safu hii,
No comments:
Post a Comment