Enter your keyword

Culture for Life.

Thursday, February 7, 2013

Uzuri ni Maisha


Kuna kitu ambacho kinawagusa vijana na wazee kwa mpigo. Kitu hicho ni Uzuri. Muonekano wa mtu wakati fulani unaweza kukita uzuri kwenye upendo kwani jinsi mtu anavyofanana huchukua sehemu kubwa na muhimu katika suala la uchaguzi wa mwenza. Hivyo msemo wa , “Uzuri upo katika jicho la mtazamaji”. Ina maana kuna kitu kinachonekana. Magerezani siku hizi hupenyezwa vioo kwa lengo moja tu, kujiangalia wenyewe. Iwe mwanamme au mwanamke, kujiona / kujihisi umependeza ni tamanio la kila binadamu.
Hivyo ninawakaribisha kwenye safari hii ambayo tutaweza kuchunguza vipengele mbalimbali vinavyohusiana na urembo, moja hadi lingine. Kama mnavyoona, uzuri wa ndani ni muhimu sana katika maisha, lakini huwa hatuuoni kwa kutazama kwa haraka au kwa mara moja. Sisi huona uzuri unaonekana kwa upande wa nje (umbile) ambao pia ni muhimu. Kama ilivyo kwa wachungaji na washauri wengine pamoja na walimu wa kiroho tunataka kutafuta ufumbuzi wa uzuri wa nje ili kujenga uwiano na ndio sababu tunasema Uzuri ni Maisha.


Uzuri ni nini …. Ni sifa ya kupendeza jicho. Sasa nywele zako zinaweza kupendeza na uso wako pia, kucha zako zinaweza kupendeza, miguu yako hali kadhalika na hadi ngozi yako pia inaweza kupendeza. Na hivi ni vile vinavyoweza kuonekana na mtu yeyote. Sasa je, ni jinsi gani wewe unaweza kuja kujiona u mzuri? Ni nini hasa kinachotakiwa kutoka kwako hadi ufikie ile hali ya kuonekana mzuri na kumvutia mtazamaji? Ni nini hasa cha kutoka kwako hata juu yako kufikia hatua ya kusema, “Naaamm, mimi ni mzuri”? Hadi wewe mwenyewe unajiona umependeza, basi ni dhahiri unajisikia vizuri. Lakini je wewe huamka tu asubuhi na kujiona umependeza? Je wakati unapotembea ni ghafla unabadilika na kuanza kupendeza? Sidhani kama ni hivyo. Kuna mtu ambae amesababisha kupendeza kwako. Lazima utakua umeenda mahali ambako wanahusika na masuala ya kupendezesha sio? Kwa sababu huwezi kwenda hospitali na kutoka na kucha zilizopakwa rangi vizuri. Hutoingia ndani ya duka kubwa lolote na kutoka na nywele laini zilizooshwa na kunyooshwa. Hali kadhalika huwezi kufanya vitu hivi jikoni kwako. Kwa vitu hivi unakwenda sehemu maalum iitwayo SALUNI
 

Sasa basi, Saluni ni nini? Kwa ujumla ni mahali ambapo wanawake na wanaume wanakwenda kupata huduma ya zinazohusiana na mitindo ya uzuri wa nywele, kucha na mwili mzima wakati wametulia. Hii inaashiria kwamba watu ambao utawakuta sehemu hiyo watakua na uwezo na watakua na muda wa kukufanya utulie na ujisikie uko nyumbani ingawa sehemu yenyewe sio nyumbani kwako. Watu hawa ni wa muhimu sana katika masuala ya uzuri. Sasa kabla ya kuzungumzia huduma utakazozipata hadi kufikia kupendeza kwako, tuangalie kwanza ni nani ambae tutataka akupatie huduma. Ni akina nani hawa, hivyo matarajio ni nini? Je wana sifa za aina gani kabla hujawakabidhi hazina yako yenye thamani sana. Ndio, kitu chochote kinachohusiana na uzuri wako ni hazina yako.
 Kitu cha kwanza na cha muhimu mtoa huduma awe na elimu juu ya kile atakachokufanyia. Lazima awe na uzoefu na huduma hiyo. Hii ni muhimu iwapo lengo la kupendeza linataka kufikiwa. Usiridhike na kufurahia huduma ambayo kesho yake itakugharimu na kukuletea majuto. Hakikisha mtu atakayekuhudumia ana uzoefu na ujuzi wa kile atakachokufanyia
 

 Ushauri – mtoa huduma lazima awe na uwezo wa kukuuliza taarifa zinazohusiana na matibabu ya awali ambayo ulishayapata. Hii ni muhimu kwa sababu kuna matibabu mengine ambayo yakichanganywa na ya aina nyingine yanaweza kusababisha sumu. Hivyo ni haki yako kuwa na wasiwasi na mtoa huduma ambae hatakudadisi kuhusu historia yako na badala yake ataendelea kutoa ushauri unaohusiana na vitu vya kufanya au ambavyo usifanye kuhusiana na tiba ulizozipata awali
 Mtoa huduma mzuri ataweza kuelezea wazi na kukuelewesha kikamilifu mtiritiko mzima utakaohusiana na mchakato wa kukupendezesha na kwamba sio
mazingaombwe. Maneno mazuri ni sawasawa na kuchua roho. Iwapo kila kitu kinawasilishwa sawasawa unaweza kutulia na kufurahia huduma zenyewe. Iwapo mtoa huduma atajieleza vizuri, kazi inakua rahisi zaidi na wateja wote wataweza kuhudumiwa kwa usawa.
 

 Mtoa huduma awe mfano mzuri wa usafi utakaojumuisha kucha zilizokatwa vizuri, mkono misafi ambayo haining’inii mapambo ya vito, awe na mavazi ya kujisitiri, na avutie makundi yote ya watu.
 

 Kipimo kikuu cha mtoa huduma mzuri ni uwezo wa kufanya kazi yake kwa makini bila ya kumfikiria mteja aliyeondoka au ambae atakuja. Lazima akoleze na alenge mawazo na juhudi yake kwa mteja aliopo wakati ule. Maisha yake ya binafsi yasiingiliane na kazi yake. Unapokwenda salon unaweza kupumzika na kuongelea maisha yako lakini hii haimpi nafasi mtoa huduma ya kuanza kukuelezea shida zake. Ni wajibu wake (mtoa huduma) kukusaidia au kukufariji au kukufurahia lakini hali hii haimpi mtoa huduma haki ya kuyasambaza mazungumzo hayo. Siri za mteja lazima ziheshimiwe wakati wote bila kujali wao ni nani.
 

 Ifuatayo inaweza kuleta mabishano lakini ni ukweli ambao usemwe. Mtoa huduma mzuri hatokuruhusu umuamrishe nini, lini, kipi na vipi kuhusiana na vitu atakavyotumia kwenye tiba yako. Yeye ndio mtaalam hivyo ni yeye wa kukueleza na kukushauri kutokana na mahitaji yako. Usihatarishe uzuri wako kwa kubahatisha. Kwa vile vitu fulani vimemsaidia mteja fulani haimaanishi ya kwamba vitakusaidia na wewe pia.
 

 Utaujua ukweli na ni ukweli huo ndio utakuweka huru. Mtoa huduma mzuri atakueleza ukweli hata kama ukweli huo utakuongoza kwenye kutokufanya huduma ambayo wewe unaitaka. Hii inadhihirisha ya kwamba mtoa huduma mzuri halengi kwenye utengenezaji pesa peke yake bali pia anafikiria hatima yako kutokana na maamuzi ya haraka na mepesi unayotaka kuyafanya. Ni lazima akueleze faida na hasara za huduma husika.
Kwa kifupi sasa unawaelewa watu ambao utawakuta ndani ya salon na hivyo unaweza kuwa na mategemeo kwamba utaridhika na huduma utakazopata. Uelewa huu utakusaidia kufanya maamuzi iwapo unataka kuwa mteja (client) au mshitiri (customer). Kila wakati jiangalie iwapo wewe ni mteja au mshitiri.
Mteja ni yule anayekwenda kwa mtaalam kwa madhumuni ya kupata ushauri wa kitaalam na hatimaye kuajiri huduma za huyo mtaalam. Mteja haruki kutoka mlango mmoja hadi mwingine. Mteja ana umiliki wa sehemu

Mshitiri ni mtu anayetafuta huduma ya aina fulani bila kujali atakapoipata. Yeye anachokitaka ni huduma. Mshitiri hana umiliki wa sehemu

Imetayarishwa na Russell Davies Touch

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu