Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, December 10, 2016

JINSI YA KUBADILI MUONEKANO WA SOFA LAKO.

Mitindo ya mito unayotumia.

 Kwasasa si wakati wa kutumia vitambaa kuremba kochi lako au Sofa ,tumia kava za mito tofautitofauti ikiwa unasofa la rangi moja,Kwa ushauri ni vema kutumia kitambaa cha rangi moja katika sofa zako kwani itakupa urahisi katika kulifanya sofa lako kuonekana vema.Tumia mito mitatu kwa sofa moja kulingana na ukubwa unaotaka.Pia ni vizuri kujua ukubwa wa mito itakayo endana na sofa lako.Pia kwa wale wenye sofa zenye rangi au maua mengi jitahidi kutumia kava za mito ambazo rangi zake zita endana na sofa lako.Ikiwa utakuwa na foronya nyingi za kubadilisha itakusaidia kulipa sofa lako mvuto mpya kila unapobadilisha.

Badilisha vitako vya sofa lako.

Kuanzia mwaka 2003  kila muundo wa sofa ulikuwa na  umbo la duara ama pembe nne,Jaribu kuangalia je vitako vya sofa lako vina muundo gani,ukisha tambua kuwa bado muundo ni uleule toka umenunua sofa lako jaribu kumpelekea fundi,kisha utakuwa na muonekano mpya wa sofa lako.

Tengeneza kava za kuvalisha sofa zima.

 Unaweza kutengeneza kava kubwa linalotosha sofa lako na kulipa muonekano mpya kulingana na rangi unazopenda.Sofa kava husaidia sana hata kwa wale ambao huofia kununua vitambaa vinavyohitaji usafi. Hasa mtu mwenye familia.

Pink Sofa cover

 

Animal Print Sofa Cover.

Tumia vichwa vya misumari{nailheads}

Utakapompelekea fundi ataelewa ni kama mapambo ya chuma ambayo huzungushiwa katika kochi wakati mwingine hata katika fanicha za dani kama vitanda,meza na makabati hutumia hivi vichwa vya misumari kama mapambo.Utaangalia ni wapi unataka kupambia lakini huwa vina pendeza sana katika viegemeo vya sofa.
 kwa mahitaji ya pillow cover na sofa cover email.abnerytupokigwe@gmail.com





No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu