Ijue Asili Na Namna Ya Kuvaa Pajama(pjs)#pajamas
By
SINYATIBLOG
On
October 21, 2017
In
Ubunifu
Mpenzi msomaji Wa makala zangu Za mavazi,leo napenda ujue asili ya vazi hili la pajama ambalo kwa sasa kutokana na mwanadada Zari kulivaa , limeshika mashiko sana Tanzania kwa wapenda fasheni .japo kuna watu walimnanga alipovaa kwa kutojua ni vazi lilioanza kuvaliwa tangu mwaka 2006 kama vazi la mtoko hata ofisini na mtani{casual wear} katika nchi za wenzetu.
Pajama ni neno lililotoholewa kutoka lugha ya uajemi(persia) na kutumika katika lugha ya kingereza huko India. vazi hili asili yake ni India na lilikuwa linavaliwa na jinsia zote pamoja na rika zote,vazi hili huvaliwa wakati Wa kwenda kulala tu usiku.Ili mwili uwe mwepesi kutokana na wepesi wa vazi lenyewe
vazi hili kwa baadhi ya nchi toka mwaka 2012 linapigwa marufuku watu kulivaa sehemu za Makutano,ofisini,na hata njiani. Vazi hili ni mahususi kwa kulalala inagawa kwa sasa ndiyo habar ya mjini.
Zari katika vazi la Pajama(pjs) |
Joketi ndani ya Pajama(pjs)
Vazi hili lilianza kuvaliwa mwaka 1870 kama vazi la kulalia huko India.Mwaka 1886 ulaya wakaanza kulivaaa nao kama vazi la kulalia. kutokana na baridi iliwabidi kutafuta vitambaa vinavyo kidhi joto.Mwaka 2006 watu wakaaza kuvaa kazini ikakatazwa kwani ilionekana wanawake wanavaa kwa lengo la kuonesha miili yao.kwasababu vazi la pajama humuweka mtu huru hivyo hafai kuvalia chupi ili uwe huru unapolala.vazi hili kwa baadhi ya nchi toka mwaka 2012 linapigwa marufuku watu kulivaa sehemu za Makutano,ofisini,na hata njiani. Vazi hili ni mahususi kwa kulalala inagawa kwa sasa ndiyo habar ya mjini.