Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, December 10, 2016

MIKOBA YA VITENGE NA UBORA WAKE.

By On December 10, 2016

Picha ya baadhi ya wallet zilizotengenezwa kwa vitenge,Kitenge ni vazi ambalo humpendeza mtu yeyote bila kujali uraia wake .


Mabegi haya ya mgongoni huweza kutumika na wanafunzi kuanzia msingi hadi chuo kikuu katika taifa letu na ikasaidia kuinua kipat cha mtanzania endapo tutaacha kasumba ya kupenda vitu kutoka n'je na kuthamini vitu tunavyotengeneza wenyewe nchini.


Mikoba hii huweza kutumika wakati wa shopping ukiwa umeweka vitu vidogovidogo kama mwanamke na ukapendeza zaidi kuliko kubeba mikoba ambayo iko common.


Huu mkoba umetengenezwa kwa kutumia vipande tofauti vya vitenge ambayo vimeufanya mkoba huu kuonekana wakipekee zaidi.





Wallet ya mtoko,valia nguo ya rangi moja kati ya rangi zilizopo hapo katika kitenge.


Mkoba wa kompyuta  bebe{Pocket laptop}


Mkoba huu ulikuwa wa rangi moja ila umenakishiwa na kipande cha kitenge.


 Mikoba hii mitatu ina  maumbo yanayo- karibiana,yote huweza kutumika  pale unapotoka kwenda sehemu,mf.sehemu ya sherehe,unaweza kutumia mikoba hii kuweka vitu vyako na ukapendeza na kuonekana mwanamke nadhifu.



JINSI YA KUBADILI MUONEKANO WA SOFA LAKO.

By On December 10, 2016

Mitindo ya mito unayotumia.

 Kwasasa si wakati wa kutumia vitambaa kuremba kochi lako au Sofa ,tumia kava za mito tofautitofauti ikiwa unasofa la rangi moja,Kwa ushauri ni vema kutumia kitambaa cha rangi moja katika sofa zako kwani itakupa urahisi katika kulifanya sofa lako kuonekana vema.Tumia mito mitatu kwa sofa moja kulingana na ukubwa unaotaka.Pia ni vizuri kujua ukubwa wa mito itakayo endana na sofa lako.Pia kwa wale wenye sofa zenye rangi au maua mengi jitahidi kutumia kava za mito ambazo rangi zake zita endana na sofa lako.Ikiwa utakuwa na foronya nyingi za kubadilisha itakusaidia kulipa sofa lako mvuto mpya kila unapobadilisha.

Badilisha vitako vya sofa lako.

Kuanzia mwaka 2003  kila muundo wa sofa ulikuwa na  umbo la duara ama pembe nne,Jaribu kuangalia je vitako vya sofa lako vina muundo gani,ukisha tambua kuwa bado muundo ni uleule toka umenunua sofa lako jaribu kumpelekea fundi,kisha utakuwa na muonekano mpya wa sofa lako.

Tengeneza kava za kuvalisha sofa zima.

 Unaweza kutengeneza kava kubwa linalotosha sofa lako na kulipa muonekano mpya kulingana na rangi unazopenda.Sofa kava husaidia sana hata kwa wale ambao huofia kununua vitambaa vinavyohitaji usafi. Hasa mtu mwenye familia.

Pink Sofa cover

 

Animal Print Sofa Cover.

Tumia vichwa vya misumari{nailheads}

Utakapompelekea fundi ataelewa ni kama mapambo ya chuma ambayo huzungushiwa katika kochi wakati mwingine hata katika fanicha za dani kama vitanda,meza na makabati hutumia hivi vichwa vya misumari kama mapambo.Utaangalia ni wapi unataka kupambia lakini huwa vina pendeza sana katika viegemeo vya sofa.
 kwa mahitaji ya pillow cover na sofa cover email.abnerytupokigwe@gmail.com





MAMBO AMBAYO HOUSE GIRL HUYAFAHAMU KULIKO MAMA MWENYE NYUMBA.

By On December 10, 2016
Wanawake wengi kwa asilimia kubwa huwaachia wadada wa ndani majukumu  ya nyumbani,hata wakati mwingine kazi wanazopaswa kufanya wao, dada wa ndani hufanya,Katika mtaa mmoja niliokuwa nikiishi kuna dada wa ndani ambaye alikuwa rafiki yangu,dada huyo alikuwa akinisimulia mambo mengi kuhusiana na mama mwenye nyumba.Jambo lililonishangaza ni mama mwenye nyumba kumpa dada wa ndani nguo zake za ndani pamoja na nguo za mmewe.Yule binti anasema "huwa nafua nguo za ndani za mama na baba",Hapa mwanamke ukiibiwa mume wako utamlaumu nani?.
Leo naomba nitaje mambo machache ambayo wadada wa ndani wanayafahamu katika usafi wa nyumba kuliko mama mwenye nyumba.

Kama house girl anatandika hivyo kitanda, wewe mwanamke mwenye nyumba ni kuamka na kuondoka, utaacha kuibiwa kweli


 Jinsi ya Kutumia Mkate.

Mkate ni kifungua kinywa ambacho hutumika na  watu wengi.Wat hupendelea kutumia mkate wakati wa asubuhi.Kuna siri kubwa sana nyuma ya mkate,naweza ukatumika katika kusafishia picha za ukutani na kava{cover} la kitabu.Hakikisha  unaloweka kidogo ili usiwe mkavu sana au nyunyuzia maji kwa mbali lakini kwa mikate milaini unaweza safishia bila kuuloweka.




Jinsi ya kusafisha  Chupa ya chai{Thermos}.

Tumia maganda ya mayai{kaka ya yai} baada ya kuyapasua kisha weka ndani ya chupa changanya na vinegar au Limao acha kwa masaa kadha au lisaa limoja kisha tikisa kama uoshavyo chupa.baada ya hapo osha vizur kwa maji safi na sabuni na kuikasha.


Usafishaji wa kabati.

   
Ni vema kusafisha  kwa kutumia dawa kabati  lako la nguo pamoja na droo,sehemu unayoweka nguo hata mara moja au mbili kwa mwaka.Hii itasaidia kuzuia wadudu kama mende kutozaliana na kutaga mayai katika kabati lako.kisha panga kabati lako katika mpangilio mzuri.kama nichupi au boksa,suruali,magauni jua sehemu ya kuziweka ili wakati wa kutafuta nguo ya kuvaa usivurugue kabati zima nakuliacha katika muonekano mbaya.



Jinsi ya kuondoa uchafu bafuni hata katika masink.

Tumia kikombe kimoja cha limao{vinegar} kisha changanya na vikombe vitatu vya maji,baada ya hapo anza kusafishia masink yako  vizuri.

Friday, December 9, 2016

NJINSI YA KUTUNZA NGOZI YAKO

By On December 09, 2016

 Kuosha uso mara kwa mara

Watu wengi huosha uso asubuhi na usiku lakini ni vema kuosha uso wako na maji safi bila hata kutumia vipodozi vya kuoshea uso kama vile  (Cleanser).usiku wakati wa kulala tumia maji safi tu ya baridi kuondoa mafuta na vipodozi ulivyojipaka usitumie cleanser usafisha uso wako tena.Kitendo cha kuosha na sabuni zenye kemikali hata zisizo na kemikali hupelekea uso kujikunja na kuonekana kama mtu mwenye miaka mingi.

Kuosha uso na maji ya moto.

Hakikisha una osha uso kwa maji ya uvuguvugu,unapotumia maji ya moto sana  huondoa mafuta ya asili katika ngozi yako pamoja na fati na acid inayopatikana katika ngoz yako.Jitahidi kuosha uso wako kwa maji ya uvuguvugu.

Kufanya skrabu mara kwa mara.

Hakuna mwanamke siyependa sura yake ivutie,lakini unapofanya skrabu mara kwa mara au mama 2 au 3 kwa wiki hupelekea ngozi yako kuwa kavu na kuonekana kuchoka.

MWANAMKE ULIYE KATIKA NDOA UNAPASWA KUFANYA HAYA.

By On December 09, 2016
Ndoa kwa kipindi hiki kwa wanawake wengi imekuwa ni kilio kila kukicha,Wanawake wengine wamekuwa wakiogopa hata kuingia katika ndoa kwa kuwa na hofu nakuona bora kupata mtoto na kumlea mwenyewe.Tukumbuke kuwa malezi ya baba na mama kwa mtoto ni muhimu kuliko malezi ya mzazi mmoja. Kuna mambo ambayo yakifayika katika familia yanaweza kumsaidia mwanamke yeyote aliyekatika ndoa.Nitajaribu kuorodhesha mambo baadhi ambayo kama mwanamke ukiyazingatia ndoa yako itakuwa imara: 


  1.Usikubali kuwa tegemezi 

Hapa na maanaisha usikubali kuwa mama wa nyumbani ,huku ukimtegemea na kumwachia mumeo majukumu yote ya kifamilia.Hata kama mwanaume anakupenda sana usikubali kuwa gori kipa tu kukaa nyumbani kwani mtegemea cha nduguye hufa masikini.Wajane wengi wanateseka sasa hivi kwasababu wengi wao waliwategemea waume zao.Zinduka mwanamke. 

2.Kuwa karibu na familia ya mumeo.

Hili ni jambo la msingi kwa mwanamke yeyote yule,wanawake wengi husahau kuwa mwanaume aliyenaye anatakiwa pia kuijali familia yake,wapo wanawake ambao huchukia endapo mwanaume anampenda mama yake mzazi au anapokuwa karibu na ndugu zake,Kumbuka kuwa unapokuwa na upendo na familia ya mumeo ni vizur zaidi hata kama hiyo familia haina shukrani wewe onyesha upendo tu.


Msanii Diamond  na Zari wa kiwa na mtoto wao Tiffa.


 3.Mpende na kumtii mumeo.

Wanaume wengi walio katika ndoa wanalalamika kuwa mwanamke akisha pata mtoto upendo huamia zaidi kwa mtoto karibu asilimia 50 ya upendo wa mke kwa mme huamia kwa mtoto,Jambo hili si jema kwani hupelekea mwanaume kuchepuka kwa lengo la kupata faraja.Hivyo mwanamke mtii mmeo na upendo wako kwake usipungue.


 4.Hakikisha watoto wako wanapata elimu.

Elimu ni Akiba salama,Unapomuelimisha mtoto kwa sasa hapo baadaye atakusaidia kwani elimu ni urithi tosha kwa mtoto wako.

 5.Mridhishe mumeo katika sekta zote mfano kimwili,kiuchumi na kiroho.

Tendo la ndoa wengi walio katika ndoa huona kwamba kwasababu amekwisha olewa basi hana haja ya kuwa mbunifu tena kwani lengo lake limetimia,kweli hapo tunakosea mwanamke unapaswa kuwa mbunifu kila siku mpe vionjo vipya mmeo,jitume kiuchumi fanya kila uwezalo kuinua kipato cha familia yako bila kusahau kuwa muombaji kwani mwanamke ndiyo mlinzi wa familia.

 
6.Mkigombana suluhisha na mumeo kabla ya kufikisha kwa wazazi. 

 

7.Muombee mumeo na pia jiombee upate kibali mbele zake.

MAGAUNI MAREFU YA VITENGE YANAYOWAVUTIA WANAWAKE WA KIAFRICA.

By On December 09, 2016

 MSANII JACQUELINE WOLPER NDANI YA MAX DRESS.





ELIZABETH MICHAEL a.k.aLULU  ndani ya Vazi la kitenge.




MITINDO MIKALI YA VITENGE MWAKA 2016.....

By On December 09, 2016

Koti refu la kitenge humpendeza mtu mwenye umbo lolote lilie,koti hili unaweza vaa hivyo na gauni fupi la rangi moja,suruali rangi moja na top rangi moja au iliyipo katika kitengeau unaweza kuvaa suruali ya kitenge cha koti na shati la rangi moja. kisha ukajipamba na mapambo yanayoendana na kitenge chako,kama vile hereni,mkufu,bangili,na hata kiatu.Vazi hili unaweza vaa:

  1.  kanisani ikiwa koti lako linafunga hata kwa kifungo kimoja,

  2. Unaweza kuvaa kwenye pati kwa kuachia kifungo bila kufunga.

Unaweza vaa hivi kwa mtoko,familia yako inaweza kupendeza hivi kwa piece mbili  na nusu za vitenge,nunua kitenge cha doti 3,


Add caption

Mpenzi msomaji wa makala zangu za mitindo ya vitenge jitahidi kushona mshono unaoendana na umbo lako,Wengi hupenda mishono mizuri wakiamini watapendeza pia kabla ya kushona shauriana na fundi wako vilevile  ni vema kufahamu rangi zinazokupendeza.

Tuesday, November 17, 2015

KEEP IT SIMPLE IN BLACK AND WHITE OUTFITS

By On November 17, 2015


kristine  Turn heads with a body con two toned black and white dress.

Ashle Madewke

BANTU MEN IN AFRICAN STYLE

By On November 17, 2015






Tuesday, September 29, 2015

WASANII WA BONGO MOVIE WAIBUKIA MJINI IRINGA,WATANGAZA KUTEMBEA NCHI NZIMA KWA BAJAJ KUMUUNGA MKONO DKT MAGUFULI

By On September 29, 2015
Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-IRINGA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.



Saturday, July 25, 2015

KANDAMA MALUNDE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA WANAHABARI SHINYANGA

By On July 25, 2015
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo.
Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugezi wa Malunde1 blog akipongezana na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician (kulia)

Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club).                                                                                                                                                                                       
Kadama Malunde Mwenyekiti Mpya wa Wanahabari Shinyanga

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga

CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC) jana Julai 23, 2015 kimefanya Uchaguzi wake Mkuu wa viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambapo mwanahabari, Kadama Malunde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Mkuu wa SPC uliofanyika mjini Shinyanga, David Nkulila alisema, Malunde ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu ambao ni Patrick Mabula, Marco Mipawa na Greyson Kakuru.

Kadama Malunde ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM na Mkurugenzi wa Malunde1 blog ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN).

Nkulila aliwataja viongozi wengine wapya waliochaguliwa kuwa ni Stephen Wang’anyi akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Shaaban Alei kuwa Makamu Mwenyekiti, Katibu Msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.

Baada ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu hiyo, kuachana na tofauti zillizokuwepo wakati wa uchaguzi na badala yake kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika klabu hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya wa SPC, Kadama aliwashukuru wanachama wote wa chama hicho kwa kumkubali aweze kushirikiana nao kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanahabari mkoani hapo pamoja na kuleta maendeleo kwa klabu hiyo. Aidha aliahidi kutenda haki kwa kila mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika utendaji wa kazi za chama.

Kwa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Felician amewataka viongozi wapya wa klabu hiyo kuendeleza misingi ya ushirikiano waliouacha na kuwasisitiza kufanya kazi kwa uwazi na ukweli huku wakizingatia maadili ya wanahabari.

Wednesday, July 22, 2015

FIVE TIPS ON HOW TO GROW EYELASHES

By On July 22, 2015


  1. 1. Using a volumizing mascara or lengthening and thickening mascara are the first step you take when you want to redeem your lashes. While waiting for them to grow look for a very good brand of mascara.
  2.  Vegetables and whole grain are really good for the body and the eyelashes, you can also take biotin and vitamin A or E multi vitamin capsules as they are known to increase growth.
  3. Good eyelashes conditioning products work also asides from helping growth, they reduce damaging, they are healthy and soft. one of the recommended lashes is NutraLuxe Lash MD.
  4. Another thing to use are eyelashes enhancers, Products like M2lashes Eyelash Activating Serum are really good. just make sure you read thoroughly and check the review and rating of any eyelashes enhancer you want to purchase.
  5.  You can also go the natural way by using castor oil mixed with either egg white or glycerin. if you are using Glycerin use 2 drops of glycerin in a 1/2 a teaspoon of castor oil. Also pure petroleum jelly like Vaseline can do a lot of work.

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu