Enter your keyword

Culture for Life.

Friday, December 9, 2016

MWANAMKE ULIYE KATIKA NDOA UNAPASWA KUFANYA HAYA.

Ndoa kwa kipindi hiki kwa wanawake wengi imekuwa ni kilio kila kukicha,Wanawake wengine wamekuwa wakiogopa hata kuingia katika ndoa kwa kuwa na hofu nakuona bora kupata mtoto na kumlea mwenyewe.Tukumbuke kuwa malezi ya baba na mama kwa mtoto ni muhimu kuliko malezi ya mzazi mmoja. Kuna mambo ambayo yakifayika katika familia yanaweza kumsaidia mwanamke yeyote aliyekatika ndoa.Nitajaribu kuorodhesha mambo baadhi ambayo kama mwanamke ukiyazingatia ndoa yako itakuwa imara: 


  1.Usikubali kuwa tegemezi 

Hapa na maanaisha usikubali kuwa mama wa nyumbani ,huku ukimtegemea na kumwachia mumeo majukumu yote ya kifamilia.Hata kama mwanaume anakupenda sana usikubali kuwa gori kipa tu kukaa nyumbani kwani mtegemea cha nduguye hufa masikini.Wajane wengi wanateseka sasa hivi kwasababu wengi wao waliwategemea waume zao.Zinduka mwanamke. 

2.Kuwa karibu na familia ya mumeo.

Hili ni jambo la msingi kwa mwanamke yeyote yule,wanawake wengi husahau kuwa mwanaume aliyenaye anatakiwa pia kuijali familia yake,wapo wanawake ambao huchukia endapo mwanaume anampenda mama yake mzazi au anapokuwa karibu na ndugu zake,Kumbuka kuwa unapokuwa na upendo na familia ya mumeo ni vizur zaidi hata kama hiyo familia haina shukrani wewe onyesha upendo tu.


Msanii Diamond  na Zari wa kiwa na mtoto wao Tiffa.


 3.Mpende na kumtii mumeo.

Wanaume wengi walio katika ndoa wanalalamika kuwa mwanamke akisha pata mtoto upendo huamia zaidi kwa mtoto karibu asilimia 50 ya upendo wa mke kwa mme huamia kwa mtoto,Jambo hili si jema kwani hupelekea mwanaume kuchepuka kwa lengo la kupata faraja.Hivyo mwanamke mtii mmeo na upendo wako kwake usipungue.


 4.Hakikisha watoto wako wanapata elimu.

Elimu ni Akiba salama,Unapomuelimisha mtoto kwa sasa hapo baadaye atakusaidia kwani elimu ni urithi tosha kwa mtoto wako.

 5.Mridhishe mumeo katika sekta zote mfano kimwili,kiuchumi na kiroho.

Tendo la ndoa wengi walio katika ndoa huona kwamba kwasababu amekwisha olewa basi hana haja ya kuwa mbunifu tena kwani lengo lake limetimia,kweli hapo tunakosea mwanamke unapaswa kuwa mbunifu kila siku mpe vionjo vipya mmeo,jitume kiuchumi fanya kila uwezalo kuinua kipato cha familia yako bila kusahau kuwa muombaji kwani mwanamke ndiyo mlinzi wa familia.

 
6.Mkigombana suluhisha na mumeo kabla ya kufikisha kwa wazazi. 

 

7.Muombee mumeo na pia jiombee upate kibali mbele zake.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu