Enter your keyword

Culture for Life.

Friday, June 12, 2015

MITINDO YA VITENGE 2015.

By On June 12, 2015

REMBA NDIYO HABARI YA MJINI KWASASA USIPITWE,UNAWEZA KUTUMIA VITAMBAA VYA SATINI,VElVET,LACE,KITENGE n.k

MFANANO WA WANANDOA.

By On June 12, 2015





Hongera Wilfred Pastory na Queen Boaz (Mr&Mrs.Mushi)


Mambo matano ambayo wanandoa hufanana wanapokuwa pamoja kwa mda mrefu;
  1. Wewe na mpenzi wako kuwa na lugha binafsi(private language).Kadri wenza watumiavyo lugha binafsi hii huonesha kiasi gani huwa na furaha pamoja.Huweza kuitana majina ya utani ikiambatana na kutaniana.Hii hali hufanya mapenzi yao kuwa na furaha na yatofauti.
  2. Kuacha kujialaumu/kujikosoa(self-censoring).Ni wazi kuwa tunapokuwa tunaongea na rafiki,ndugu na jamaa huwa tuazungumza kwa kuangalia mazingira uliyopo lakini upozungumza na mpenzi wako uliyemzoea huwa unakuwa huru kuzungumza kama kawaida(Naturaly)bila kujali mazingira/unajiachilia.
  3. Mazungumzo hufanana(You start to sound alike)Watu waliokaa pamoja kwa mda mrefu ,wakati mwingine watu husema hufanana hadi sura,Ukweli ni kwamba watu hawa hufanana kimsamiati hata mpangilio wa sentensi zao huwa sawa.
  4. Hufanana.Wanandoa na wapokaa kwa pamoja kwa mda mrefu na kufanya vitu vingi pamoja hupelekea wao kufana.
  5. Kuwa na utani uliopitiliza.Wenza huweza kuelewana kwa ishara hata vitendo kabla ya mazungumzo kwasababu wanaelewana vema hata kwa kutazamana huweza kuzungumza yote inatokana na kukaa kwao kwa kipindi kirefu na kujuana vema,wakati mwingine huweza kutaniana na watu wanao wazunguka wakaona kuwa si utani lakini wao huona kawaida kwasababu wanaelewana vema.

Wednesday, June 10, 2015

NDOA NDOANO KATIKA JAMII....

By On June 10, 2015


Image result for tendo la ndoaImage result for tendo la ndoa
Katika safu hii nitazungumzia vitu vichache vinavyowafanya watu wasifurahie tendo la ndoa .Hapa nazungumza na wanandoa na wanaoelekea kungia katika ndoa.Leo tuangalie mambo baadhi kwa ufupi:
  1. Kuongelea matatizo wakati wa tendo la ndoa.Hapa mwanaume/mwanamke unapoona mwenzi wako anahamu na wewe baadala ya kusoma alama za nyakati wewe unaanza kuongelea shida zako,za ndugu hata majirani wakati mwingine mnaanza kukumbushiana majeraha mlio wahi kukwazana.Hii hali itawaoondoa katika raha mlio taka kuipata.Hapa sasa mmoja wapo anapotoka n’je na kukutana na mtu mwenye kusoma alama za nyakati utaipenda kwasababu utampoteza mwenza wako na hatokuwa na shauku na wewe.
  2. Kusumbuliwa na jinni mahaba,hili ni tatizo linalowakabiri wanandoa wengi hukosa hamu ya kufanya mapenzi na wenza wao hata kama alikuwa na shauku akiwa safarini kwamba nikifika mke/mme wangu basi leo nitafurahi lakini anapo mkaribia hamu ina isha.Watu wenye tabia hiyo jua anasumbuliwa na jini mahaba na baadhi ya dalili zao nikuota ndoto wanafanya mapenzi kwenye ndoto,kupoteza pete,kufunga harusi wakiwa katika ndoto n.k.Ukiona hivi wewe ingia katika maombi na ujitenge na hizo roho.
  3. Kutokuwa na Lugha ya mahaba .Wanaume/wanawake wengi huogopa kujiachilia na kumwambia mwenzi wako jinsi unavyojisikia,kuwa wazi kwa mwenzi wako usione aibu unapokuwa naye katika tendo la ndoa.Toa hata kiasauti kidogo hii itamfanya mwenzi wako kuona kuwa unamjali na mko pamoja hata unapo wahikufikia mshindo/kileleni usikae kama bubu endelea kumtia moyo mmeo/mkeo ikiwezekana mwambie aongeze kasi au apunguze mwambie unavyojisikia utamfanya aone kuwa bado una mpenda na akikukumbuka basi atakumbuka sauti zako na kuwa na hamu na wewe.
  4. Uchafu wa kitanda na chumba chetu.Hapa mwanamke ni jukumu lako kufanya chumba chenu kiwe kisafi mda wote.Wanawake wa siku hizi huu utandawazi utatumaliza na kuharibu ndoa zetu hasa tunapo waachia wadada wa kazi kufanya usafi wa chumba chenu.Mwanamke hakikisha huwaruhusu hata watoto kuingia chumbani kwako.kuwa na tabia ya kubadili shuka kila siku mumeo atavutiwa na kubadilisha muonekano wa chumba chako sio kila siku kitanda kina kaa kwenye dirisha au ukutatani.
  5. Uvivu wakati wa tendo la ndoa.Wanawake/wanaume wengi ni wavivu mwanamke usimwachie mumeo kukushughulikia tu wewe ukiwa umekaa kama gogo,wengine ukoroma kabisa hata kulala,hii huonesha dharau kwa mumeo pia wanaume wengine ni wavivu katika tendo la ndoa mshindo mmoja hoi,utampoteza mkeo ,wengine watakusaidia kazi.Mwisho kabisa napenda kuwaomba wanaume/wanawake kuzingatia usafi wa miili yetu  ikiwa ni pamoja na kunyoa nywele za makwapani,sehemu za siri na kusafisha vinywa vyetu  vizuri vilevile tupotaka kufanya tendo la ndoa  mkiweza nendeni hata bafuni muoge pamoja.Wanawake wenzangu ni vema ukiwa msafi zaidi na kujua kusafisha sehemu zetu vema hata kutumia vitu vya kuondoa harufu katika makwapa au vinywa vyetu ili waume zetu wasitukimbie.

FAIDA YA TENDO LA NDOA.

By On June 10, 2015


Image result for tendo la ndoa
Nitumaini langu wewe unayesoma makala hii ni mwanandoa au upo katika harakati za kuingia katika ndoa.Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa hufanywa na wana ndoa tu na siyo wachumba,marafiki na halifanyiki hovyohovyo tu bila makubaliano ya watu wawili nikiwa na maana ya wanandoa.
Image result for tendo la ndoa
1.Tendo hili ni muhimu kwani hufanya ndoa iendelee kuwepo.Ndiyo sababu wanandoa mmoja wapo anapokosa kupata ushirikiano kwa mwenza wake.hupelekea ndoa kuvunjika na kufanya mmoja wapo kutoka n’je ya ndoa.

2.Tendo la ndoa ni burudani kwa wanandoa.Wakati mwingine mtu anayekosa kufanya tendo hili katika ndoa hupelekea migogoro hata kununiana ndani ya nyumba,kuwa na msongo wa mawazo.

3.Hapa wanandoa wanatakiwa kuwa wavumilivu na kujitoa.

4.lengo hasa la tendo la ndoa ni uzazi.Ili kuikamilisha ndoa lazima mpate watoto ndiyo sababu ya kuunganika na kuwa mwili mmoja.Kwasasa tendo la ndoa limekuwa likifanywa.kinyume,wengi wetu katika jamii wanafanya bila kuzingatiaa maadili ya hili tendo,mzee kwa kijana,mume au mke wa mtu,vijana,watoto walio chini ya miaka 18 pia wamejiingiza katika zinaa(Uzinzi).Mpenzi msomaji kama wewe ni mmoja wapo tulia kuwa na mmoja ambaye ni mume au mke wako ndiyo utafurahia tendo la ndoa.

JINSI WAZAZI WANAVYO WAHARIBU WATOTO .

By On June 10, 2015



Uelimshaji wa mtoto ni jukumu la kila mtu.Kumbuka kuwa moja ya vitu vinavyowachanganya watoto ni makuzi ya watoto katika mazingira wanayo lelewa.Leo katika safu napenda kuzungumzia baadhi vipengele ambavyo vitamuweka mtoto wako katika mazingira mazuri ikiwa wazazi watazingatia haya katika kuwa sahihisha watoto na wakuwarekebisha.

  1. Image result for watoto

    Usahihishaji wa dhana au maneno katika kuyaelewa na kuyatamka.mfano

     

Mtoto- Mtoto anaona mtoto wa Punda kisha anamwambia mama Mbwa.Hapa wazazi wengine huitikia ndiyo Mbwa bila kujua kuwa anampotosha mtoto.Mama ilitakiwa aseme hapana  ni mtoto wa Punda.Hapo mtoto wakati mwingine hatosema Mbwa anatasema mama Punda.

  1. Urekebishaji wa tabia,kukemea na kupongeza.Mtoto mwenye tabia ya kutukana anapaswa kukemea na anapokuwa na tabia nzuri anapaswa kupongezwa.
  2. Mpangilio sahihi wa maneno.(Sintaksia ya watoto)Mara nyingi wazazi hawazingatii urekebishaji wa makosa ya kisarufi kwa watoto zaidi huzingatia maana .Kimsingi mtoto anapaswa kufundishwa namna ya kupangilia maneno katika sentensi na katika matumizi ya nyakati.Mfano.
              Mtoto- Juma ataenda shule jana.
               Mtu mzima- Juma alienda shule jana.kumbuka kuwa mtoto mdogo anauwezo mkubwa wa kujifunza lugha kuliko mtu mzima.Hivyo basi mtoto anaporekebishwa akiwa mdogo hatoweza kukosea tena.






JINSI MTU MZIMA ANAVYOWEZA KUUTEKA USIKIVU WA MTOTO.

By On June 10, 2015

.
Image result for watoto

Mpenzi msomaji wa makala zangu, leo napenda kuwakumbusha watu wazima katika uzungumzaji wao hasa wanapo zungumza na watoto.Ifahamike kuwa siku zote mzungumzaji humtegemea msikilizaji anapozungumza.Ikiwa mtu mzima anaongea katika kundi la watoto ni vema akitumia nguvu kubwa ya ziada na kufanya yafuaatayo:



  1. Matumizi ya majina na alama za mshangao(Attention getters).Hii itasaidia kumuelekeza mtoto mazungumzo gain yanaelekezwa kwao na yapi yanayopaswa kusikilizwa.Matumizi ya majina na vichekeo hupatikana katika makundi mawili makubwa.mfano mtu mzima anapoongea na mtoto hutumia jina la mtoto la mwanzoni mfano.Irene njoo hapa,wakati mwingine hutumia alama za mshangao baadala ya kutumia majina,mfano aah! Mbona husikii. Alama hizi huwa kabla ya sentensi anyotaka kusema.
  2. Matumizi ya Vichekeo(Attention holders stimulus)vinavyovuta hisia.Hivi hutumika pale mzungumzaji anapotaka kuzungumza jambo zaidi ya moja.Mfano anaposimulia  hadithi.
  3. Ubadilishaji wa sauti(Attention holder)katika kipengele hiki kuna vitu vifuatavyo:Uzungumzaji wa sauti ya juu kwa watoto,mtu mzima huongea kwa sauti ya juu sana hasa anapoongea na mtoto wa miaka miwili,miaka mitano sauti ya juu kiasi..
  4. Unong’onezaji.Mtu mzima hutumia sauti ndogo ya kunong’oneza na watoto wao hasa wanapowalisha au anapombembeleza ili alale.Watu wazima hunong’oneza hasa wanapoongea na watoto wa miaka 2-5 lakini wanpozungumza na watu wazima hawa nong’oni.


Thursday, May 21, 2015

Jinsi ya Kuuteka Upendo Wa Mama Mkwe.

By On May 21, 2015

Wanawake wenzangu wengi wetu tumekuwa tukiwachukia wakwe zetu kwa kauli za kusikia tu kwa watu.Tabia za wakwe zetu kweli huwa hazilingani wapo wenye upendo wa dhati lakini wengine utajuta hata mume utamkimbia.Leo naomba tusaidiane kidogo ili kuweza kuifurahia ndoa yako pamoja na kumpenda mkwe wako zaidi kwa vitu vidogo ambavyo havina gharama lakini vitakupa heshima na kupendwa na mama mkwe.
  1. Jifunye kunyenyekea kwa mama mkwe kwa lolote unalifanya juu yake au wewe unapo kuwa naye.
  2. Mama mkwe muone kama mama yako mzazi.Mpende kama mama yako aliyekuzaa na kuwa wazi kwake.Jitahidi kumjua kuwa anapenda nini? ili unapoweza unamnunulia na kumpa.
  3. Msifie mumeo mbele kwake,pia mwambia jinsi gani una mpenda mmeo,siyo kumpa lawama na madhaifu ya mumeo.Mambo mengine mnasuluhisha wenyewe siyo lazima kuyafikisha kwa ndugu.
  4. Si vema kuishi nyumba moja na mama mkwe kama si lazima ili kuepuka lawama na ugomvi usio na tija.
  5. Usimwite mume wako jina lake mbele ya mkweo.Itaonesha kuwa unamdharau.
  6. Tumia fedha vizuri ukiwa unaishi na mama mkwe nyumba moja pamoja na kuwa mwangalifu jinsi unavyoshi na mumeo,epuka vitendo ambavyo ni chukizo kwa mama mkwe.
  7. Penda kumzawadia unapokuwa naye hata unapokwenda kumtembelea.
  8. Mfanyie vitu ambavyo hata mama yako mzazi hujawahi mfanyia mridhishe nakumfurahia kwa yale mema anyofanya hata kama machache.
  9. Jifunze kusamehe na kusahau pale anapokukosea.Pia mtumaini Mungu sana siku zote za maisha yako.
  10. Muoneshe upendo siku zote.Nitumaini langu kuwa umeelewa ,tafadhari toa maoni yako,pia mshirikishe mwanamke mwenzio juu ya hii mada ili iwe msaada kwa wengi.Toa maoni yako hapo chini......Usisite kutoa comment zako itasaidia wengine pia.

JINSI YA KUPANGA MIKAKATI BORA KATIKA FAMILIA YAKO.

By On May 21, 2015



Leo katika safu hii ya maisha na mahusiano naomba tukumbushane haya,Katika jamii zetu tunaona kila siku matatizo wanayo kumbana nayo wanawake wajane.Mwanaume kumbuka wewe ndiyo msingi au kichwa cha familia,Hivyo basi kama mwanaume yakupasa kutafakari na kufanya haya katika familia yako.
  1. Mfanye mke kuwa mrithi wa mali zako.Pia hakikisha umemwandika mkeo katika nyaraka za urithi wa mali zako.
  2. Mke wako anapaswa kufahamu miradi yako
  3. Hakikisha mali zenu zina majina yenu wawili au ya watoto.
  4. Mwanaume ufanye kazi kwa bidii ili kuweza kulea familia yako.
  5. Uwe na mapenzi ya dhati kwa mkeo na kutokukubali watu,ndugu na marafiki kuwa tenganisha.
  6. Wapende wanao na kuwapeleka shule  ili baadaye waweze kujitegemea na walee katika maadili mema ya dini.
  7. Kuwa mwaminifu kwa mkeo.
  8. Kutomsema mkeo vibaya kwa ndugu na jamaa zako,Msifie mkeo kwa ndugu na jamaa na kutosema udhaifu wake.
  9. Kuwa na akaunti moja wewe na mkeo.
  10. Mkeo mpe uwezo wa kufanya kazi na kuweza kujitegemea .

Monday, May 11, 2015

MIKOBA NA VIATU VYA KITENGE.

By On May 11, 2015

Kiatu cha Kitenge au Mkoba na Hereni unaweza kutengeneza hata wewe ukiwa nyumbani na kubadilisha kiatu kilicho choka au mkoba ulio choka na kuwa mpya.Vitu unavyopaswa kuwa navyo ni vitendea kazi tu, kama gundi ya simba,kiatu,mkoba na mkasi


AFRICAN PRINTS KWA WATOTO.

By On May 11, 2015



Saturday, May 9, 2015

VYAKULA AMBAVYO MAMA MJAMZITO HAPASWI KUTUMIA.

By On May 09, 2015

Mjali mwanao.

Mama Mjamzito waweza kula kwa mpangilo huu.

  1. Mlo wa Asubuhi:    A - Chungwa/ Embe/ Ndizi mbivu/ Parachichi,  B - Mkate/ Maandazi/ Chapati/ Vitumbua,Uji      C - Karoti    D - Mayai,    E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya  Soya
  2. Mlo wa Mchana:     A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na chungwa,  B - Ugali/ Wali/ Ndizi/ Makande/ Tambi          C - Mchicha/ matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji,      D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa        E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya  Soya.
  3. Mlo wa Usiku:        A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na Chungwa,   B - Wali/ Ndizi/ Viazi/ Tambi/ Chapati          C - Mchicha/ Matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji,      D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa           E - Maziwa/Mtindi/Siagi/Maziwa ya  Soya.
  4.  

Vitu na Vyakula vya kuepuka mama mjamzito.
  • Matumizi ya Pombe wakati wa ujauzito huathiri mtoto. Hurusiwi kutumia pombe.
  • Uvutaji Sigara
  • Kupunguza unywaji wa kahawa au vinywaji vyenye caffeine nyingi.
  • Samaki aina ya papa, swordfish, tilefish na king mackerel kwani wana mekuryi kwa wingi ambayo ni mbaya kwa afya

MADHARA YA KUFANYA TENDO LA NDOA KINYUME CHA MAUMBILE.

By On May 09, 2015

Mjali mwenzi wako.

MOJA, Njia ya haja kubwa haina vilainishi/lubrication asilia kama jinsi Uke ulivyo.huwa inasababisha kuchubuka kwa tisu/ngozi laini ndani ya njia ya haja kubwa hiyo, na hivyo kupelekea michubuko ambayo bacteria, virusi na hata vimelea vingine kuweza kupenya wakati wa majeraha hayo ya michubuko na hivyo kuingia katika mfumo wa damu kupitia majeraha hayo.Hii inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa pamoja na VVU.
Tafiti zinaonyesha ya kuwa Ngono kwa Njia ya haja kubwa ipo katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa zaidi ya asilimia 30% kuliko watu wanaotumia njia ngono kwa njia ya Uke.Vile vile mtu anakuwa katika hatari kubwa ya kupata virusi vya human papillomavirus (HPV ) ambavyo huweza kumpelekea mtu anayejihusisha na ngono kinyume na maumbile kupata muwasho katika eneo hilo la haja kubwa na hata kupelekea kupata kansa.


PILI, Tishu ndani ya njia ya haja kubwa, haijakingwa na kulindwa kwa ngozi ngumu kama ilivyo sehemu za nje za mwili. Tishu zote za nje ya miili yetu zina ngozi ambayo ni seli zilizokufa ambazo hutusaidia kutukinga dhidi ya maabukizi ya vimelea na vile vile hutulinda na vitu tofauti katika mazingira.Hivyo ndani ya njia ya haja kubwa hakujakingwa na ulizi huo wa asili wa seli hizo ili kuweza kuhimili, hivyo kuifanya iwe katika hatari kubwa ya kusuguliwa na hivyo kuchanika ambayo hupekea kusababisha maambukizi kuwa rahisi kutokea.
Pia ngozi ndani ya njia ya haja kubwa iko tofauti na ile ya ukeni ambapo ngozi ya ukeni huweza kuhimili ile misuguano pasipo kuweza kusababisha michumbuko kwa sababu ya vilainishi asili vinavyoatikana ndian ya uke na gozi husika.

TATU, Njia ya haya kubwa ni Maalumu kupitisha Kinyesi tu.Kwa jinsi ambavyo njia hii imeundwa ama kutengenezwa ni maalumu kwa kuhimili na kupitisha kinyeshi tu na si vinginevyo.Njia ya haja kubwa imezungukwa na kama misuli mfano wa ringi ama kwa kitaalamu huitwa (Anal sphincter) ambayo kazi yake ni kukaza eneo hilo kabla na baada ya kujisaidia tu.Kipindi ambapo misuli hiyo (anal sphincter)imekazwa ama kubwa kwa kuingiziwa kitu kingine kigumu huweza kusababisha maumivu makali kwa muhusika.Inapoendelea kuwa na mrudio wa mara kwa mara wa ufanyaji wa Ngono kwa njia hii ya haja kubwa ama kinyume na maumbile hufanya misuli hiyo ya njia ya haja kubwa kuwa dhaifu ama kulegea na isiwe na uwezo tena wakukaza kama kazi yake inavyotakiwa kufanya. Na hivyo kuwa vigumu kuweza kuzuia kinyesi kuweza kupita mpaka utapokuwa tayari kuweza kukitoa hivyo kusababisha utokaji ovyo wa kinyesi

.NNE, Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi.Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi sana tofauti na Ukeni kulivyo hata kama wapenzi hawana maambukizi yeyote ya zinaa au ugonjwa wowote bacteria huwa wapo tu eneo hilo na hawa ni bacteria wa kawaida (Normal flora). Mtu anapokuwa naingiza uume ndani ya njia ya haja kuwa anakuwa anaingiza vimelea vingine vya bacteria katika eneo hilo na wanapokutana na wale bacteria wengine waliopo katika eneo hilo husababisha madhara.

Pia pale unapohamisha uume toka katika njia ya haja kubwa na kupeleka katika Njia ya Uke badi bacteria hao utawapeleka katika eneo Uke ambapo Njia ya haja kubwa inakuwa na bacteria wengi na hivyo kupelekea maambukizi ukeni na pia maambukizi katika njia mkojo.Ngono kwa njia ya haja kubwa inaweza kusababisha madhara mengine kwa afya ya watu wanaojihusisha na Njia hii ya ngono na wanaweza kupata madhaara kama haya yafuatayo,


Pale mdomo unapogusana na njia ya haja kubwa au kugusa uume uliotoka kwenye njia ya haja kuwa kwa mdomo kunaweza kupelekea kupata kwa wote mtu na mpenzi wake kuwa katika hatari ya kupataa magonjwa ya HEPATITIS C, HERPES/ malengelenge, kupata virusi vya human papillomavirus (HPV) na maambukizo mengine.


Hata hivyo, majeraha makubwa wakati wa ngono kwa njia ya haja kubwa mara nyingine ingawa sio kila mara hali hii kutokea inaweza kupelekea Damu kuvuja kwa ndani (hemorrhoids) baada ya tendo hilo kufanyika ambalo inaweza kusababisha au kupasuka ama kuchanika kwa misuli/nyama ndani ya njia ya haya kubwa kwa sababu ya msuguano mkali na muda mwingine hupelekea kuweza kutoboka kwa utumbo mpana(colon) hii huweza kwa ni tukio la hatari zaidi ambalo huhitaji msaada wa kitabibu haraka kwa matibabu na hata kufanyiwa upasuaji zaidi na hata kupoteza maisha kunaweza kutokea.




TANO, pia kwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao kushindwa kuhimili kukaza kwakati wa kusukuma mtoto na hivyo inaweza kupelekea utokaji wa kinyesi wakati wa kusukuma mtoto. jambo ambalo huleta tabu kwa wahudumu wa afya kwa kutumia muda mwigi kuwahudumia.Njia pekee ya kuepuka kabisa hatari hizo za ngono kinyume na maumbile ni kuacha kabisa ngono kwa njia hiyo ya haja kubwa.shiriki katika ngono kwa njia ya kawaida na ikibidi kwa kutumia kondomu ili kujilinda dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa.Kuepuka kuingiza uume ndani ya uke na kisha mdomoni ikiwa uume ulikuwa umeingizwa katika njia ya haja kubwa.Tuzingatie maadili ya dini zetu na utamaduni wetu bila kusahau kujali afya yako.














 

GAUNI LAKO LA HARUSI

By On May 09, 2015

MITINDO MIKALI YA VITENGE 2015

By On May 09, 2015

Remba ndiyo habari ya mjini kwa Tz ingawa wa Nigeria walianza kitambo,ila kwa sasa ndiyo imekamata rika zote hasa kwenye shughuli za sherehe..


kitenge kimechanganywa na kitambaa kinachovutika.

Suruali ya Kitenge simple with pemplum top

Solo ya style ya kitenge iliyokatwa kimtego,unaweza vaa popote kulingana na mazingira.Hapa kila shape inapendeza.

Iro$Buba ya kitenge ushindwe wewe.

Gauni la  kitenge solo staili


MISHONO YA VITENGE

By On May 09, 2015

Gauni la shift la kitenge waweza vaa popote ila kulingana na mazingira.

Mtindo huu wa kitenge una weza valiwa na watu wasio na matumbo makubwa.

Mtindo wa kitenge kwa mtoko zaid.

Wavulana mtoko simple wa kitenge.


Shati la makenzi.


Tupokigwe Abnery ,hereni nime buni   mwenyewe ushindwe ww tu kupendeza ndani ya Batiki.


3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu