Enter your keyword

Culture for Life.

Sunday, January 29, 2017

Kufanya Scalp Husaidia Nywele Zako Kuwa Zenye Afya

By On January 29, 2017

Haikikisha unafanya scalp  na mafuta sahihi ya nywele zako,Scalp husaidia nywele kukua,unachotakiwa kuifanya  ni kuchukua  mafuta ya nazi kuzipaka nywele zako kisha fanya scalp ya kichwa kwa kutumia vidole vyako kisha  osha nywele zako kama ulivyozoea ,itakusaidia pia kupunguza stress  ikiwa nywele zako ni fupi pia itaongeza mzunguko wa damu.

"Use your fingertips and a bit of Argan or coconut oil to rub in a circular motion for several minutes before you shampoo," says John Masters, owner of John Masters Organic Salon. 



Viatu Unavyoweza Kuvaa na Leggings

By On January 29, 2017

Knee-high boots with leggings




 

Buti huweza kuvaliwa hasa wakati wa baridi hupendeza zaidi unaweza kuvaa buti zako na taiti ndefu.Hapa utaangalia mtindo gani wa buti unapendelea wewe.Vilevile unaweza kuvaa buti ya rangi moja inayofanana na tight yako kisha uvaa soksi za rangi nyingine ilikuweka mvuto zaidi na kuweka laini itakayoonyesha mwisho wa soksi zako na buti pamoja na tight yako inapoanzia.

 Sandals with leggings.

Sendoz huvaliwa hasa kipindi chenye joto lakini pia wanawake wengi hupenda sana sendo kwani ni rahisi kuvaliwa na mavazi yoyote itategemea tu wewe umejipangilia vipi.


Sneakers with leggings

Sneakers zinavaliwa sana na jinsia zote mbili pia wana mitindo wengi wamekuwa wakizitumia sana katika maonyesho ya mitindo,Ukivaa leggings yako na sneakers utavutia zaidi na kuonekana bado kijana ikiwa unaogopa kuwa ni za vijana.










Flats with leggings
kwa muonekano mzuri unapo vaa skintight yako ni vema kuangalia skin unayo iva kama ni ya rangi moja pamoja na top rangi moja hakikisha unatupia kiatu chako flat chenye maua au mchanganiyiko wa rangi.Viatu vilivyoflati ni vizuri pia kwa mtu asiwe weza viatu viatu virefu au anaye kwenda umbali mrefu hata kwa safari vunafaa pia.




 

Aina 10 za Wanaume Wanaokera Wanawake.

By On January 29, 2017


1. Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband).
HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband).
Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.

3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband).
Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.

4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband).
 Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.

5. Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband).
Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao.

6. Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband).
Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena.

7. Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband).
 Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.

8. Mume Mtalii (Visiting Husband). 
Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.

9. Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband). 
Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.

10. Mwanaume Mbahili (Miserly Husband).
Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.
Source Mungwanablog.

Friday, January 27, 2017

Mtindo wa kutoboa kucha " Kim Kardashian's"

By On January 27, 2017

Inavutia lakini je kwa wewe mwanamke ambaye unategemewa kwa majukumu ya nyumbani usithubutu kufanya hivi.Hii ni kwakina dada ambao wanafanyiwa kazi nyingi kama kuosha vyombo,kufua,na kazi zingine hasa za kutumia maji kwa kusugua.

Paris Couture Week:" More picture of KENDALL JENNER"

By On January 27, 2017

Thursday, January 26, 2017

Handmade fabric neckwear "Mtindo rahisi na mpya wa kuwa na Necklace simple"

By On January 26, 2017



Kadri siku zinavyosonga mitindo mipya inayotokana na vitenge,kente,bongolan na vitambaa vingine vya Kiafrika vinazidi kutafutiwa makeke ya kufanya mtu apendeze.
Hivi sasa unaweza kushona neckwear au mkufu wa  shingoni kwa kipande kidogo cha kitenge na ukavutia zaidi.Nashauri wewe kama ni fundi usitupe masalia ya vitenge,hata mtu unapoenda kushona hakikisha hutupi kitenge kwasababu tu kimebakia kidogo.

Hizi chini ni baadhi tu ya mitindo ya neckwear ila unaweza kubuni utakavyo.

Designed by barefoot modiste.

Njia 6 Zitakazo kufanya uvutie na Mikufu ya Kiafrika(African Necklace)

By On January 26, 2017

  •  kuwa na mkufu wenye rangi nyingi au maua ya rangi tofauti,ikiwa unavaa nguo yenye rangi moja. 

    Zulu beads Necklace

  • Kuwa na mkufu ambao utaweza kuvalia vazi lako la usiku
  • Angalia urefu wa mkufu wako unaohitaji.Kulingana na wewe ulivyo ,mtu mfupi mkufu mrefu kwake huwa ni mzuri zaidi hufanya avutie zaidi na kumrefusha lakini pia anaweza kutumia kulingana na hitaji lake
  • Hakikisha unakuwa na Mkufu ambao unaweza kuuvaa asubuhi mpaka usiku,kwasababu mikufu  mingine hutegemeana na mda unaovaa,huenda umenunua mkufu wa usiku wewe unauvaa asubuhi. 
  • Jitahidi kuwa na mkufu mmoja unao fanana na moja ya nguo zako.
  •  Wakati mwingine unaweza kuvaa mikufu miwili tofauti kwa wakati mmoja kwa lengo la kuvutia tu muonekano wako.
  • Unajua kuwa nguo inyokufanya unang'aa ni nguo nzuri kwako kwani ukufanya uonekane mdogo pia mwenye afya.Bado nasisitiza kuwa mavazi ya kiafrika huvutia sana ikiwa tu utajipangilia vema.


Wednesday, January 25, 2017

Njia 7 za kuwa Mume bora kwa Mkeo Mwaka 2017

By On January 25, 2017
Ni wazi kuwa suala la ndoa kwa sasa ni kilio kwa wengi,Kila mtu ana namna ambavyo analichukulia suala hili,Ukisoma katika magazeti,kusikiliza redio,katika blog na kusikiliza mahubiri yana mtaka mwanamke kusimamia ndoa yake ili isiharibike,Ingawa sijafikia hatua hiyo lakini bado naona katika jamii yangu jinsi ambavyo wanawake wameachiwa majukumu mengi.


Leo naomba wanaume mtambue mchango wenu katika ndoa kwa kufanya haya:

Endelea kumpenda kwa kasi ile ile

Kumbuka wakati wa uchumba jinsi mlivyokuwa mkiishi,unamtumia ujumbe mzuri katika simu yake,pamoja na kumwambia maneno mazuri wakati wote unapokuwa karibu naye au mbali naye,mitoko mikali una mpa zawadi, Ulikuwa una mfanya akuamini hata unapokuwa mbali naye.Hayo mambo uliyokuwa ukiyafanya hata sasa yana nafasi yake  na hata kama ndoa ilianza kuingia dosari utakapo fanya tena kwa kasi nyingine hakika ndoa yako itakuwa na furaha.

 

Kuwa msikivu na muulizaji wa mambo unayotaka majibu yake.

Ni kweli kwamba wanawake wanapenda kusikilizwa kwa umakini,ikiwa mkeo anazungumza na wewe na wewe unakuwa na michakato yako, lazima ataona kuwa unamdharau,Hapo lazima atajisikia vibaya na kuona kuwa kitu anachozungumza hakina faida.Hivyo basi kama mwaka 2016 hukuweza kufanya hivyo sasa ni wakati wako,Anapoaaza kuongea na wewe basi zima simu au weka mbali na wewe ,Tv zima au Punguza sauti.Hata asipotaka kukuambia  mwambie mke wangu nahitaji kujua umefikia wapi katika biashara zako,kama anasoma muulize,uliza vitu unavyoamini anavifanya ,basi huenda hata hujui hata kimoja muulize swali la ujumla ili afunguke.

 Kuwa mbunifu katika tendo la ndoa.

Hapa watu husahau kuwa tendo la ndoa ni muhimu kwa wanandoa,Muulize mkeo anapendelea nini katika tendo la ndoa mitindo gani anapenda,hata wakati mwingine badilisheni mazingira ya kufanyia sex,sehemu moja kila siku inachosha na kupunguza hamasa ya kufanya tendo lenyewe siku moja mfanyie suprise mama watoto toka hata n'je ya nyumba nendeni hata hotelini au mazingira ya nyumbani hapohapo kwa kutegemea mnaishije kama na familia lazima muwe makini lakini kama mpo wawili basi sehemu ni nyingi.Pia mwanaume jua sehemu zinazo mfanya mke wako afurahie tendo la ndoa ,hujui basi google kwasababu wanawake wengine si rahisi kuongea.

Tumia busara katika kutatua ugomvi.

Kuwa na mda wa kuzungumza na mke wako.

Ndiyo nyakati hizi za sayansi na teknolojia inasababisha pia wanandoa kugombana kwani mda mwingi hutumika katika simu au kompyuta na kukosa mda wa kuzungumza na mkeo.Ni vema kutenga mda wa kuzungumza na mwenzi wako kuliko kuwa busy mda wote na mitandao.Hata kama unatafuta pesa mwanamke anapenda mwanaume anayetenga mda wa kuwa naye japo hata lisa.

Mheshimu na kumjali Mke Wako.

Hakika ukifanya haya mwanamke atakupenda,atakujali na kukuheshimu pamoja na kumuona mkeo akiwa na furaha siku zote. kama utamfanyia haya basi naye ataongeza upendo zaidi kwako hata kufanya yale ambayo ajawahi kukufanyia ili mradi nawe ufurahi.

 


 

Tuesday, January 24, 2017

Maswali ya Msingi Ya Kujiuliza Kabla Hujamwamini Mtu.

By On January 24, 2017

Je,Namwamini huyu mtu kwa  kiasi gani kwa mazungumzo yake au namna anavyofikiria mambo kwa undani.

llustration: Julia Breckenreid
  •  Je, Mtu huyu anaelewa jambo ninalotaka kulizungumzia.

  • Je,Mtu huyu anapenda mafanikio yangu.

  • Je,Mtu huyu yupo tayari kunieleza ukweli wakati wote.

Maumivu Ya Mwanadamu Hujificha Sehemu Hizi:

By On January 24, 2017

Katika mifupa ya Miili yetu.

 

Wakati mwingine mtu huwa na maumivu makali hata ya uchovu au misongo ya mawazo pamoja matatizo yatokanayo na changamoto za maisha.Maumivu huweza kujificha katika moyo,mgongoni,kiuno ,miguuni na sehemu zingine za mwili lakini unapofanya mazoezi hali hiyo huisha kabisa.

Nyimbo

Najua unaposikia baadhi ya nyimbo huku kumbusha wakati wa raha na wakati uliopitia shida.Sasa wakati mwingine unapokuwa umetulia na kuuusikia wimbo ambao uliusikia ukiwa katika majonzi  lazima akili yako itakurudisha hali ilivyokuwa kipindi hicho.

 Daftari la kumbukumbu

Unapopitia daftari la kumbukumbu zako lazima utakumbuka baadhi ya mambo yaliyokuumiza na kukufanya uwaze au uanze kutafakari hali ilivyotokea mpaka kuisha kwake.Ni vema kuto kuhifadhi kumbukumbu zinazoumiza moyo wako.

Mazingira tuliyoishi na watu wa karibu yetu

Mfano ulizoea kukuaa na mtu sehemu fulani za kupumzika inapotokea amefariki au mmetengana,unapopita hizo sehemu lazima utamkumbuka na kutamani kuwa naye ikiwa sehemu hiyo mlifanya jambo la heri au mlizungumza mengi mazuri,Kama sehemu hiyo ilikuwa na ugomvi huwezi kuikumbuka na kuifurahia.

Wednesday, January 18, 2017

Mtindo Mpya wa Mavazi ya Kiafrika na "Jewelry designer Gbenga Artsmith",

By On January 18, 2017
VAZI LA KIAFRIKA LILILOSHONEWA SHANGA KAMA  MZUNGUKO WAKE NA KUUPA MUONEKANO MZURI.

Jewelry/Styling: Gbenga Artsmith | @gbengaartsmith
Photography: Francis Lens | @francislens
Makeup/Headwrap: Olamide | @bolams
Costume: Hadassah Clothings | @hadassahclothings and Abike Clothings | @abikeclothings
Model: Cynthia | @cynthia_diko
Source: BellaNaija.com

Sunday, January 15, 2017

How to Rock Your Outfit with African Necklace,

By On January 15, 2017















OUTFIT DETAILS:
Picture Joy Kendi,Kenyan fashion Blogger.
Plain Black Tee: F&F
High Waist Sheer Skirt: Made by my tailor. Tailor: (+254)723813011
Massaii Choker: Maasai Market CBD
Top Neck Piece: Identity SA
Foral Neck Piece: Romwe.com

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu