Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, January 7, 2017

Aina za Wanaume Unaotakiwa Kuonana nao Lakini sio kuolewa nao.

Ni kweli kuna wanaume unatakiwa kuonana nao katika maisha yako lakini si wanaume ambao wanapaswa wakuoe  hata kama umewapenda sana ,Watu wazima husema weka mbali na watoto.

#1:Mwanaume anayefahamiana na watu wengi mjini.

Huyu ni mwanaume ambaye ni maarufu ambaye hakuna mtu asiye mfahamu,hakuna sehemu maarufu za starehe hazifahamu hadi wenye madaraka mahali hapo yeye anawafahamu,hakuna kampuni haijui au mtu ambaye hamfahamu hapo.Basi mwanaume kama huyu ni vizuri kuwa rafiki yako,kwani hata kama unahitaji kazi basi yeye anaweza peleka maombi yako na ukapata kazi,unahitaji ukumbi,nyumba au viwanja au unashida kituo cha polisi unaweza kuta anawatu anawajua kituo cha polisi,hata wanasheria anawafahamu yaani yeye mji anaufahamu pamoja watu katika sekta muhimu anawafahamu.Mtu kama huyo mda wote yeye huwa yuko busy kuchati na watu ni mpenzi wa kila mtu.Basi ni vema akiwa rafiki yako na asiwe mume wako.Naamini unatambua kwanini sisemi awe mume wako.

#2Mwanaume mwenye muonekano mzuri au tajiri na aliyefanikiwa sana.

Huyu ni mwanaume ambaye hata ukipita naye barabarani hata rafiki zako hushindwa kukwepesha macho, humtamani na kumuangalia kwa macho mawili.Mwanaume kama huyu atakusaidia hata unapokuwa  na shida,hutapata tabu  ingawa ni vigumu kuzuia hisia kwa mwanaume kama huyo kwa njia yoyote jitahidi awe rafiki tu.Katika ndoa kuuzuia wivu ni vigumu sana basi hata ukijizuia still mnaweza kwaruzana kwa vitu vidogo,Kumbuka kitu kizuri hupendwa na wengi.

#3Mwanaume  mwenye mvuto na mwenye umri mdogo au mkubwa kwako.

Wakati mwingine unaweza kukutana na mwanaume ambaye ana umri mdogo kuliko wewe au mkubwa,Mkawa marafiki  kwa kubadilishana mawazo lakini mkawa na mahusiano ya karibu na akawa kama mfariji kwako hasa wakati ambao wanawake wengi mnapitia magumu,tukiacha wakati wa raha,hata kama huwezi zuia hisia zako jitahidi awe rafiki lakini asiwe mume wako wa ndoa.

#4Mwanaume mcheshi,mchangamfu ,asiyejua kukasirika mda wote yeye ni mwenye furaha.

Mwanaume kama huyu hata unapomkosea yeye huwa kimya ,ni vema kuwa naye kama rafiki kwani wakati mwingine unaweza mkosea akawa kimya lakini,Uwazi katika mahusiano ni jambo la msingi kwani mtu asiye ongea wala kuzungumza unapomkosea lazima atakupa hofu hata kuzungumza naye jambo lolote.Hapa utajifunza suala la uwazi katika mahusiano yako.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu