Sikweli kwamba mwanamke mwenye picha nyingi kwenye mtandao hafai kuolewa.Hili suala la kutupia picha katika mitandao ya kijamii jamani wengi ni walengwa hata mimi ni mlengwa kwa kweli wengine picha ni hobby au tunapenda kupiga picha labda sehemu zile za kupumzika(washroom) tunako jifungia ndiyo tunashindwa kupiga picha.
Hapa kitu cha msingi cha kuzingatiwa ni kuendana na maadili yetu utu kama watanzania au mtoto uliyelelewa katika maadili mazuri.
Jambo hili si kwa kwa wanawake tu hata wanaume wapo wanaopenda picha sana tu na wanazitupia kwenye mitandao ya kijamii.Tutambue mabadiliko ya sayansi na teknolojia kadri yanavybadilika hata mfumo wa maisha unabadilika .kwanini nasema hivyo kwasababu hata jinsi sisi wanadamu tuishivyo si sawa na babu zetu walivyoishi.Sasa hivi dunia imekuwa kama kijiji kimoja.
Niwezacho kusema hapa ni kwamba asilimia kubwa ya watu tunatumia sana mitandao ya kijamii. wapo watu ambao hadi leo hii hawataki kutumia smartphone wakiamini kwamba ni anasa au zinawaingizia gharama je ni mpaka lini utaamni hivyo,wengine hata kuwanunulia wake zao hawataki wakiamini hii mitandao ya kijamii inachangia kuharibu ndoa, si kweli tukiamini hivi basi hata magari vyombo vya usafiri tusinge vitumia kwa kuogopa ajari.
Naomba tu kuzungumzia hizi pande mbili kwanza za uwekaji wa picha katika mitandao ya kijamii
Wanawake wanaoweka picha zao na wazazi wanao weka picha za watoto katika mitandao ya kijamii.
Utafiti unaonyesha kuwa Asilimia 63% ya wanawake ambao ni walezi wanatumia facebook na asilimia 97% ya wanawake huwa wanatupia picha za watoto wao katika facebook huku asilimia 89% huandika mambo yanayowahusu watoto wao kila mara(status) na asilimia 46% huweka video za watoto wao.
Kuna picha za watoto ambazo kwa kweli hupaswi kuzitupia katika mitandao kwa ajili ya usalama wa mtoto wakati mwingine mtoto wako kapiga picha na mtoto wa mwenzio basi kwasababu umezipenda picha hizo unazitupia facebook bila kujali kama mwenye mtoto atapenda.Mfano
Mzazi, mtoto wakati anamuogesha anatupia picha yake,
Baba anakunywa pombe basi akiwa anacheza na mtoto kwa masihara tu anamuonjesha chupa hata kama hamna kitu anampiga picha anatupia katika mtandao
Mtoto yupo juu ya poti uchi unatupia kwenye mtandao
Ameumia au anaumwa kidogo unatupia kwenye mtandao ohhh please friend pray for my son,
Hupaswi kuweka wazi habari za mtoto wako mfanfano jina kamili la mtoto,shule anayosoma hujui watu gani wanatatumia hizo details pia kumbuka kila kinachotupiwa katika mtandao huwa hakipotei.
Hata kama mtoto wako anawadhamini katika masomo yake si vema kuweka wazi katika mitandao.wanadamu hatupendani.Hili liko wazi wengine huamini kwamba kusema yote hayo ni kuwa na hofu hapana hata katika imani za dini ni kwamba nyota ya mtu huonekana tangu utotoni sasa wewe weka sana picha za mwanao kwa kila jambo analo fanya.Hata baadaye sidhani kama mwanao atapenda kuona picha aliyokuwa uchi au unamnywesha bia au kashika bia akiwa mdogo itamletea picha gani hivyo nitumaini langu umenilewa kiasi.
Upande wa kina dada sisi kina dada ni wazi kuwa tunapenda picha hata mimi ni mmojawapo,Nilileta hii mada katika ukurasa wangu wa facebook nimeona kurasa nyingi zikituzungumzia sisi wanawake juu ya uwekaji wa picha katika mitandao.Kwamba mwanamke mwenye picha nyingi katika mtandao si wa kuoa.Nikajaribu kuangalia nikaona hili jambo halina ukweli basi nikaomba mawazo ya rafiki zangu,nashukuru hawakusita kuchangia mada yangu.Ukweli ni huu picha haipelekei wewe kuoa au kuolewa na wakati mwingine watu hutumia picha ambazo si zao katika mitandao.
Jambo la msingi wanawake wenzangu hata kama tunapenda picha tujitahidi kuweka picha zenye maadili na si picha za mavazi nusu uchi au yanayoonyesha maungo yetu,Pia tuangalie vitu vya kushare katika mitandao kwani yapo mambo ni private pia yanafanyika sirini.kutokana na maoni ya marafiki zangu ni kwamba kuwa na picha nyingi katika mitandao ya kijamii hakupelekei mwanamke kuto kuolewa au mwanaume kushindwa kuoa.Tafadhari pitia comment za marafiki hapo chini:
Asante rafiki zangu wote mlioweza kucomment kile mlichoona ni sahihi,nitumaini kuna mtu atakuwa amepata kitu namna ya kutumia mitandao hii ya kijamii,Pia kuelewa kuwa heshima ya mtu hujengwa na yeye mwenyewe jinsi anavyojitambulisha kwa jamii,hivyohivyo kwa wanaume.Asante nawapenda.
Burudani : TRA na BASATA Wasaini Makubaliano ya Kubadilishana Taarifa na
Kudhibiti Mapato ya Wasanii
-
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeingia makubaliano na Baraza la Sanaa
Tanzania (BASATA) ili kubadilishana taarifa na kusomana mifumo ya kudhibiti
mapa...
1 day ago
No comments:
Post a Comment