Katika mifupa ya Miili yetu.
Wakati mwingine mtu huwa na maumivu makali hata ya uchovu au misongo ya mawazo pamoja matatizo yatokanayo na changamoto za maisha.Maumivu huweza kujificha katika moyo,mgongoni,kiuno ,miguuni na sehemu zingine za mwili lakini unapofanya mazoezi hali hiyo huisha kabisa.
Nyimbo
Najua unaposikia baadhi ya nyimbo huku kumbusha wakati wa raha na wakati uliopitia shida.Sasa wakati mwingine unapokuwa umetulia na kuuusikia wimbo ambao uliusikia ukiwa katika majonzi lazima akili yako itakurudisha hali ilivyokuwa kipindi hicho.
Daftari la kumbukumbu
Unapopitia daftari la kumbukumbu zako lazima utakumbuka baadhi ya mambo yaliyokuumiza na kukufanya uwaze au uanze kutafakari hali ilivyotokea mpaka kuisha kwake.Ni vema kuto kuhifadhi kumbukumbu zinazoumiza moyo wako.
Mazingira tuliyoishi na watu wa karibu yetu
Mfano ulizoea kukuaa na mtu sehemu fulani za kupumzika inapotokea amefariki au mmetengana,unapopita hizo sehemu lazima utamkumbuka na kutamani kuwa naye ikiwa sehemu hiyo mlifanya jambo la heri au mlizungumza mengi mazuri,Kama sehemu hiyo ilikuwa na ugomvi huwezi kuikumbuka na kuifurahia.
No comments:
Post a Comment