Enter your keyword

Culture for Life.

Wednesday, January 4, 2017

Wabunifu wa Nguo Tanzania tuongeze Ubunifu zaidi "Acheni kucopy na Kupaste"

Kanga ni vazi ambalo linatumika sana na wanawake wa Afrika Mashariki.Ni vazi ambalo mwanamke yeyote yule lazima awe nalo.Tunashukuru kwa Wabunifu wetu wa Tanzania kwa jinsi ambavyo wanajitahidi kuutangaza utamaduni wa Tanzania kupitia mitindo mbalimbali kwa kutumia vitambaa kama kanga na vitenge vitu vingine mf ngozi nk.



Leo naomba tu kusema kuwa kweli wanamitindo kadri siku zinavyozidi kusonga wabunifu wanaongezeka sana,lakini jambo la msingi ambalo sisi kama wabunifu tunapaswa kufikiria ni kwamba  tujiulize nini maana ya mbunifu,ni kweli tunapata fedha kutokana na kazi tunazofanya lakini bado kazi zetu hatuwezi kujiita wabunifu kwa sababu asilimia kubwa ya mitindo yetu ni ya kucopy na kupaste yaani kupakua na kubandika.

  Usiku wa Kanga Party katika ukumbi wa Regency Park Hotel wanamitindo walikutana katika Party hiyo iliyoandaliwa na mwanamitindo Asya Idarous Khamsin,Usiku wa tarehe 31 mwaka 2016 siku ya mkesha wa mwaka mpya.


Je? hapo utajiita mbunifu pia kazi zetu lazima ziwe tofauti ili  tuweze kubainisha huyu ni mbunifu chipukizi na huyu ni Mbunifu aliyekuwa katika tasnia ya ubunifu kupitia kazi zetu.Jaribu kuangalia mitindo mingi inayoshonwa sasa hivi hamna mtindo ambao siyo wa kupakua kutoka nguo za mastaa wa n'je ambazo zimebuniwa na wanamitindo wa n'je.Pia mitindo mingi nchini ni ile ya nchi za jirani.

Tuamke Wabunifu wa Tanzania tuwe creative tuache kupakua na kubandika.Wabunifu wetu watanzania wanafanya kazi kubwa sana lakini bado katika suala la ubunifu tupo nyuma sana.
Mwanamke uvaa vazi la kanga wakati wakupika,shambani,kwenye msiba,wakati wa kwenda sokoni mwanamke huvaa kanga ingawa siku hizi mambo yamebadilika ukionekana umejifunga kanga sokoni mfano binti unaweza kuonekana kama wa kuja lakini ni jambo la kawaida mwanamke kuvaa kanga.Kanga huweza kufungwa kiunoni kama hivyo kwa mwanamke au juu ya matiti wakati wa kwenda kuoga kama taulo.

Binafsi nawapongeza Wabunifu wakubwa waliopo nchini pamoja na chipukizi ila ombi langu ni kwamba tufanye biashara lakini pia tuumize vichwa vyetu kubuni mavazi ambayo yatatumbulisha popote tuendapo kupitia mavazi tu mtu ajulikana huyu ni mtanzania,namnukuu mbunifu Makeke yeye anakuambia  YOUR CULTURE YOUR IDENTITY.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu