Enter your keyword

Culture for Life.

Thursday, January 5, 2017

Sababu za Wanawake na wanaume Wengi kutojingiza katika ndoa Mapema.

Tamaa ya utajiri.

 

Hili ni wazi kabisa kwamba hata wanaume siku hizi wanataka kuoa mwanamke mwenye mali. zamani ilikuwa  mwanamke mwenye elimu anapendwa sana lakini sasa hivi kama mwanamke huna mali wala elimu hakuna mwanaume atakaye kupenda  au kujisogeza karibu yako.Wanaume siku hizi na wenyewe wanaolewa na wanawake wenye fedha maana nikisema wanaoa nitakuwa nadanganya.Mwanaume wa kiafrika anaolewa na mwanamke wa kizungu si kwasababu kampenda lahasha!  au binti wa kiafrika na mzungu au mwanaume aliyemzidi umri ,ana kuwa kafuata fedha za kibabu cha kizungu au mwanamke mwenye mali.Vivyo hivyo  kwa wanawake tunachagua mwanaume atayeweza kukutunza na si mwanaume suruali.Ila kumbuka kwamba penzi zuri ni lile la kutafuta wote ukiingia na mwili wako utaishia kunyanyasika tu.

Dharau

Hapa wanawake kwa wanaume kuwa na dharau ni moja ya kitu kinachoturudisha nyuma siku zote,unachagua mpaka basi,mwanamke ni tabia pia mwanaume ni tabia hahahaa... shepu inatafutwa hata uzuri unatafutwa jamani embu tutulie,Kwa kuchagua huko mara rangi,huyu mfupi,huyu mrefu sana.Hutapata suluhu ya kuingia katika ndoa.


Kuto kusali

Kila jambo bila msaada wa Mungu basi utaishia kusugua miguu na kujibadili muonekano wako bila mafaniko.Piga goti kwa imani yako muombe Mungu bila kukata tamaa pamoja na kumuomba akuepushe na wanaume wachafuzi,wakati mwingine hata kuomba huenda unakosea usiseme Mungu naomba mchumba sema Mungu nipe mume,Mungu nipe Mke,ukisema mchumba watakuja wachafua mazingira na wakimbiaji wasio oa, kazi kujielezea na kuhitaji mwili wako tu.

Mavazi yasiyo na heshima

 

Wakati mwingine mavazi ya mwanamke na mwanaume pia ni jambo la kujiangalia mwanaume uko hovyohovyo hata kujipangilia huwezi shati moja unavaa siku mbili,suruali haibanduki kutwa huko nayo hicho kiatu ndo balaa mwanaume ukimsogelea mwanamke yaani unanuka kwapa mdomo ndo usiseme.Kweli kwa mtindo huo utapata mke.Pia mwanamke wewe mavazi yako ni nusu uchi,mda wote mavazi yako yanaonyesha maumbile yako,pamoja nakutupia picha  kwenye mitandao picha za kubinua makalio kweli utaolewa au utachezewa na wapenda kubinuliwa matako.

Kujipodoa kuliko pitiliza.

Siku hizi  kinadada nawapongeza kwasababu mtaani hakuna tena wanawake weusi ukitaka kuwaona basi mpaka uwatafute kwa tochi wengi wetu tumejichubua tumekuwa weupe wote,ukiongezea na makeup ndo usiseme,Nawasifia kwa kuwa mnapendeza na ukweli ni kwamba mwanamke sharti upendeze lakini ukijipodoa ukapitiliza kwa kweli ule uasilia wako ukipotea hata uzuri wako unapotea tupunguze kidogo. Vilevile kina kaka jamani ndiyo manpendeza huko salon na nyie mnakoenda kufanya scrub hivi mwanaume wewe ushazoeana na hao wadada wafanyascrub ukirudi kwa girl wako unamwambia jinsi unavyofanyiwa na wakati mwingine unaenda naye anaona uanvyoregea mwanaume ukufanyiwa Scrub hivi mwanamke gani asiye na wivu,Ni kweli mnapendeza ila pigeni kazi mwanaume asifiwi sura bali kazi na wallet ina nini?Zinduka.



Kuto kuwa na siri katika mikakati yako

Kutokuwa na siri juu ya mambo tunayofanya leo wengi  wetu mitandao imetuharibu kila kitu unapost umefanya hiki unapost duh! ni jambo dogo lakini linaweza kukuonyesha kuwa huna siri hata utakapo olewa au kuoa,pia wanaume wengine mashauzi yamezidi kila ukikutana naye nimajisifu kuhusu mali alizonazo na wengine hawana bali mbwembwe za mjini siyo Issue.Zinduka piga kazi.

Kutokuwa na malengo

Mwanamke yeyote au Mwanaume asiye na malengo hafai,wewe kila unapokutana na mume wako mda wote unawaza ngono tu,starehe leo uende kiwanja hiki kesho kile wewe kila kiwanja unakijua.Lakini upande wa maendeleo hamna unachowaza.Kweli ukioa au kuolewa utafaa kuwa mzazi. Pia mwanaume wewe kazi yako kudhurura nyumba za wanawake kuoa huoi ila lengo lako kujistarehesha nafsi yako na kuacha,Maumivu unayo mwachia huyo mwanamke hupelekea kuwa laana na kukufanya usipate mke wa kuoa.

Kufikria vitu vikubwa kwa mwenzi wako kuliko upendo halisi.

Mwanamke na wewe Mwanaume  wakati wote unatamani mwenzi wako akufanyie jambo kubwa mfano kukunulia gari,yaani vitu vya thamani bila kujali kwanza upendo wa mpenzi wako.Kwa njia hii tusingeona wazazi wetu hapo walipo.Zinduka.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu