Enter your keyword

Culture for Life.

Monday, January 9, 2017

Wasanii Wa Tanzania Vaeni Mavazi Ya Kiafrika Kudumisha Utamaduni Wetu.

Watanzania wengi tunapenda kucopy na kupaste lakini kama wasanii wetu ndani ya nchi watathamini mavazi ya ndani ya nchi naamini watu wengi watapenda na kuvaa mavazi yanayoshonwa na wabunifu wetu ndani ya nchi.Nimejaribu kuangalia baadhi ya mavazi yanayovaliwa sana na watanzania mengi ni yale yaliyovaliwa na Wasanii wetu.

Harmonize na Jackline Wolper


Ni ombi langu kwenu wasanii wa bongo kupenda vitu vya ndani ya nchi yetu kama nchi za jirani  katika Afrika  mfano,Ghana,Nigeria,southAfrica na nchi zingine tunaona kwenye nyimbo hata filamu zao wengi wanavaa mavazi ya kiasili lakini Tanzania bado tuna Kasumba ya kupenda mavazi ya n'je vyetu tutavithamini lini?.Hata kama basi tukiyavaa haya onyeshi uasilia kwani wengi tuna vaa mavazi ya nchi za jirani  hasa Nigeria na Ghana.

Nitatupia picha za wasanii wachache ambao wakivaa mavazi ya kiasili wanapendeza:

Msanii wa nyimbo za maghani  Mrisho Mpoto na Banana Zorro.

Mrisho Mpoto ni miongoni mwa wasanii wa kiume Tanzania ambao wanathamini sana Mavazi ya Kiafrika sambamba na Banana Zorro.


Jackline Wolper,ni msanii ambaye naona anawafuasi wengi wanaofuatilia muonekano wake,hili miongoni mwa magauni yanayoshonwa sana now na wadada wengi.Kama wasanii wote watapenda mavazi ya kiasili basi itasaidia kuinua pato la taifa hasa kwa kuthamini mavazi ya ndani ya nchi yetu.

Ikiwa wasanii wote wata thamini mavazi yanayotengenezwa nchini basi itafanya hata taifa kutafuta vazi la Taifa kama nchi zetu za  jirani na kupitia wasanii wetu vazi letu litafaamika kwa haraka kwani Msanii ni kioo cha Jamii.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu