Fahamu vyakula vya msingi kwa ajili ya ubora wa nywele zako.
Unaweza kusuka mtindo huu kwa kutumia Soft Dread au Lena |
Karibu
tena mpenzi msomaji wa makala hii ya Urembo na Mitindo inayokujia kila
wiki kupitia safu hii.Katika makala hii nitazungumzia utunzaji wa nywele kwa wanaume na wanawake .Nitakutajia vyakula ambavyo hufanya nywele kuwa imara na zenye mvuto asilia,Watu wengi hulalamika nywele kukatika,kuwa nyepesi,kuwa kavu na kukosa mvuto.
Watu
wengi hupenda kutumia vyakula mbalimbali bila ya kufahamu umuhimu wa
vyakula hivyo katika miili yao.Vifuatavyo ni vyakula ambavyo hufanya
nywele zako kuwa imara, na vyakula hivi si vigeni katika maisha yetu ya
kila siku.
Maharage
yana protini nyingi kama vile zinc, biotin pamoja na madini ya chuma
ambayo hufanya nywele kuwa na virutubisho na muonekano mzuri. Maharage
ni mboga inayopendwa na watu wengi, pia ni rahisi kupatikana. Kadri unavyoitumia ndivyo nywele zako zitakavyozidi kuwa bora na imara zaidi.
Watanzania
wengi hawana mazoea ya kunywa maziwa huku wengi wakijenga imani potofu
kuwa maziwa hufaa kwa watoto wadogo pekee.Maziwa yanaprotini nyingi
ambazo husadia kutoa vurutubisho katika nywele na kuzuia kukatika.
Mayai
Mayai pia yanaprotini nyingi ambazo husaidia nywele zako kuwa imara na huzuia zisikatike
hovyo.Hata ukijaribu kuchunguza baadhi ya shampoo ambazo hutumika
kusafishia nywele huwa zimetengenezwa kwa mchanganyiko wa kemikali
mbalimbali pamoja na mayai.
Samaki
ni miongoni mwa vyakula muhimu sana katika kustawisha nywele na
kuzifanya ziwe imara na zenye muonekano mzuri. Matumizi ya samaki katika
mlo husaidia kuzifanya nywele zako kuwa imara toka kwenye ngozi hadi
kwenye ncha ya nywele kutokana na uwingi wa protini inayopatikana katika
Samaki.
Karoti
Matumizi
ya karoti kwa walio wengi hupenda kutumia kama kiugo katika vyakula na
hasa mboga.Ni vyema kutumia karoti kwa wingi kwani zina vitamin A na
hivyo zitazifanya nywele zako kuwa imara pamoja na kuiacha ngozi yako
kuwa yenye kuvutia na kuondoa ukavu wa ngozi.
Unapotumia
karoti inasaidia kuzuia kuungua ngozi wakati unapoweka dawa kichwani,
kuepusha michubuko katika ngozi, na pia huzuia kuwepo kwa mba kichwani.
Hivyo basi kama unasumbuliwa na mba, ni vyema ukatumia karoti ili
kuepukana na tatizo hilo.
Unashauriwa
kujua aina yako ya nywele iliuweze kuchagua dawa iliyo sahihi kwa
nywele zako hii itakusaidia kuepuka nywele kukatika,kuwa kavu,kuwa
nyepesi na kukosa mvuto pia ni muhimu kumtafuta mshauri wa anayejua
masawala ya nywele ili uwe na uhakika unapo tumia vupodozi vya nywele.
No comments:
Post a Comment