Tangu Juma lililopita Makeke na Studio Maisha tumeshirikiana kuandaaa project Mpya na tayari
awamu ya kwanza imefanyika na imeonekana kukubalika zaidi kwa jamii na wadau wa
mitindo, project inaitwa THE RISE OF AFRICAN QUEEN
”Jocktan Makeke alisema hasa Katika
mahojiano aliyofanya na Sinyatiblog siku ya trh 13/12/2016”
Jocktan alisema”Kuna kauli isemayo mwanamke akiwezeshwa
anaweza, kama ilivo kauli hio project hii imejikita zaidi kumsaidia mwanamke
hasa mwanamke mwenye ndoto ya kuwa
mwanamitindo wa kimataifa, Wazo hili lilikuja baada ya kuona kuwa wapo wanawake
wengi sana wenye vipaji na wana vigezo
vyote vya kuwa wanamitindo bora wa hapo badaye lakini wana kosa msaada kuhusu
wapi wataanzia na watafikaje? Kiwango cha kimataifa katika masuala ya mitindo.
Project hii inahusu wasichana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 22.Waandaaji wa Project hii ni MAISHA STUDIO kampuni inayojihusisha na
masuala ya upigaji wa Picha , na MAKEKE AFRIKA
kampuni ya mitindo ya kiasili.
Kwa kila mwezi mmoja tutakuwa tukiwatoa watu wawili ambao ni new faces, project hii imeanza na
wasichana kwanza lakini hapo badaye tutaendelea na THE RISE OF AFRICAN KINGS
ambayo itakuwa kwa vijana wa kiume tu na mwisho tutamaliza na THE RISE OF
AFFICAN KING & QUEEN hapo tutajumuisha vijana wawili kila mwezi, wa kike na
wa kiume.
Tunaamini kuwa project hii itakuwa ni fursa na mlango Mpya
kwa vijana kwani hawatagharamika kwa kitu chochote na Picha zao zitasambazwa
kwenye media zetu mbalimbali , pia
vijana kushiriliki majukwaa mbaimbali ya mitindo , kitaifa na kimataifa.
Sinyatiblog:hongera kazi nzuri na mchango wenu ni mkubwa
sana kwa jamii,je mnatarajia kushirikisha mikoa yote au ni Dar tu je taratibu
zikoje kwa mtu anayetaka kushiriki.
Jocktan: Hatulipani chochote kwasababu ni kwaajili yao, ukisema sasa hivi
umchukue mpiga picha mkali umpeleke eneo la kupigia picha, ni Pesa
nyingi sana ambazo ni ngumu
kugharamia,Kwahiyo kupitia project itakuwa bure tu na kwasasa tunaanzia Dar tu baadaye ndiyo tutafika mikoani.Vilevile Wana mitindo tumaozungumzia hapa ni modelz tu.Kwasasa tumeanza tayari na Models wawili.
kugharamia,Kwahiyo kupitia project itakuwa bure tu na kwasasa tunaanzia Dar tu baadaye ndiyo tutafika mikoani.Vilevile Wana mitindo tumaozungumzia hapa ni modelz tu.Kwasasa tumeanza tayari na Models wawili.
No comments:
Post a Comment