Maxi skirt katika muonekano wa kitenge ni mshono ambayo Mwaka 2016 hauja mtupa mwanamke ,kutoka na uwezo wa kumpendeza kila mtu bila kujali umbo lake.
Wanawake wanene,wembamba,warefu kwa wafupi mshono huu unawapendeza.Mbali na kumpendeza kila mtu mshono huu pia unamfanya mwanamke aonekane mwenye heshima zaidi.
Mtindo huu mwanamke huweza kwenda nao mahali popote { location} yoyote ikiwa hajaweka mpasua mkubwa mbele ya skirt ama pembeni.Mshono huu kwa mtu mwenye tumbo unaweza kushona belt pana na mtu mwembamba anaweza kushona belt zote mbili aidha pana au nyembamba.
Nimejaribu kuonyesha baadhi ya picha za mtindo wa skirt hizi.Ni wazi kuwa mshono huu hautapitwa na wakati hata Mwaka 2017 utaendelea kushonwa na kuwapendeza wengi.
No comments:
Post a Comment