Enter your keyword

Culture for Life.

Sunday, December 18, 2016

Jinsi ya kusafisha Unyayo

Si kitu cha ajabu katika saluni zetu kuwakuta wanawake wakisafishwa kucha  na kupakwa rangi ili kuvutia miguu yao.Usafishaji na utunzaji wa miili yetu ni jukumu letu kufanya hivyo ili kuendelea kuvutia zaidi.

Leo katika safu hii ya urembo napenda nizungumzie suala hili la usafishaji wa unyayo.Wapo wanawake au wanaume ambao miguu yao huchanika, kuwa na fangasi au kuwa  na funza kutokana  na mazingira tunayoishi na jinsi tunavyotunza nyayo zetu, wengi wetu tunajisahau katika jukumu hili la kusafisha nyayo zetu.

Zifuatazo ni njia za utunzaji wa Unyayo

Jitahidi kila siku kuosha unyayo wako kwa maji ya uvuguvugu na  sabuni, kabla hujaanza kusafisha unyayo wako weka miguu katika maji ya moto kiasi, kwa muda wa dakika 5 kisha anza kusafisha kwa sabuni.

Changanya maji yako na asali, ambayo husaidia kulainisha ngozi ya Unyayo wako pamoja na kuondoa michubuko iliyopo katika Unyayo.

Ukimaliza kuosha Unyayo wako, hakikisha unajikausha na kitambaa kikavu kuanzia katika vidole vyako. Usipo kausha vema hupelekea kupata fangasi na kupelekea miguu kunuka unapokuwa umevaa viatu vya kudumbukiza.Watu walio chanika miguu wanashauriwa kutumia viatu vya wazi kwa muda mrefu huku ukizingatia taaratibu za usafishaji wa nyayo, pia unaweza kutumia cream za kulainisha Unyayo wako ambazo hupatikana katika maduka ya vipodozi.

Pendelea kutumia mafuta ya watoto kujipaka katika Unyayo wako(baby Oil) au paka Grisalini(glyceline) kwenye unyayo kisha vaa soksi wakati wa kulala, Soksi husadia kulainisha Unyayo wako kutokana na hali ya joto  inayokuwepo ndani ya soksi.

Ongeza kiwango cha kunywa maji, kila siku jitahidi kunywa angalau lita moja ya maji  ambayo husadia  ngozi yako kuendelea kuwa  nyororo.

Comment yako ni muhimu baada ya kusoma makala hii.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu