Enter your keyword

Culture for Life.

Thursday, December 29, 2016

African home decoration

Afrika ni bara lenye utajiri mwingi sana isipokuwa watu waliondani ya nchi za Afrika wengi wetu tuna thamini vitu vya n'je kuliko ndani ya nchi zetu.Huwa najiuliza hii kasumba itaisha lini.Mbali na hivyo sisi ni waajabu hasa pale tunapopenda vitu vya ndani ya nchi endapo vitapendwa na watu wa mataifa ya n'je naweza sema huu ni ujinga wa fikra.Kuna vitu vilivyo ndani ya mazingira tuliyopo endapo akili zetu zitafunguka basi tutajivunia mali zetu.

BAADHI VITU AMBAVYO VINAWEZA KUFANYA MUONEKANO WA KIASILI KATIKA NYUMBA YAKO.

Hii ni coach lenye kava la ngozi ya pundamilia,Mnyama ambaye yupo katika hifadhi zetu za taifa.Ni fahali ndani ya nyumba yako kuwa  na vitu vilivyopo katika nchi yako.Simaanishi mtu awinde ilikupata ngozi ya Pundamilia hapana ila kwa wenye  uwezo wa kununua ngozi hizi wanaweza fanya hivyo na kubuni chochote ndani ya nyumba zao kama zuria la ngozi ya Pundamilia.Kwa mtu ambaye hawezi anaweza nunua vitambaa {animal print}na kutengenezea  mfano.sofa au pillow na mashuka pia,

 

Haya ni makopo ya maua yaliyo gundishiwa vitenge na kufanya yawe na muonekano mzuri zaidi.Unaweza badili muonekano wa makopo yako  ya maua nyumbani kwa kufanya hivi.


Muonekano wa sahani iliyo chorwa rangi za vitenge,Mwanamke unapoandaa chakula kumbuka kuwa hamu ya mtu kula huanzia katika muonekano wa n'je wa chakula chenyewe ambapo hata sahani inapaswa kumvutia mraji.Sahani hii hakika inamvuta mraji na kutamani kula chakula chako.

Kuna watu wamezoea kulalamika kuwa hawezi kuipamba nyumba yake kwakuwa hana fedha za kutosha,Binafsi napinga hilo ukiwa mbunifu nyumba yako itaonekana mpya kila siku.Hiyo picha inaonyesha maua,Leo nakupa mbinu ya kuifanya nyumba yako ivutie katika muonekano asilia.Tafuta mti mkavu urefu unaotaka  hakikisha unamatawi matawi na uwe umekauka ,kisha utafutie verse au mtungi wa maua unaweza weka mchanga ndani ya mtungi halafu unadumbukiza mti wako kama ulivyo.Ukitaka uonekane vizuri unaweza nunua spray ya rangi katika maduka ya hardware rangi unayotaka .Kabla ya kuweka kwenye mtungi unauspray n'je ili kupata muonekano unaotaka subiri kwa nusu saa kisha kaupambe ndani.


Mfagio wa chelewa unaweza badilisha muonekano wa nyumba yako.Nunua mfagio wa chelewa kisha uspray rangi utakao weka kwenye mtungi wako.


{African Print window curtain} pazia limetengenezwa kwa vipande vya vitenge ambavyo mafundi wengi hutupa wanapo maliza kushona.Unaweza kutumia vipande hivyo kupata pazia na ukaokoa gharama.



No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu