Enter your keyword

Culture for Life.

Friday, December 23, 2016

Ways to Wish Someone a Happy Holiday




Katika msimu huu wa sikukuu ni jambo la heri kumtakia heri Rafiki,ndugu na jamaa,na hata kupatana na watu uliokosana nao kwani si vema kumaliza mwaka ukiwa na maadui au watu tu ambao walikuudhi ama kuwaudhi,unaweza kuwatumia ujumbe wa heri ya kwaajili ya sikukuu pamoja na Mwaka mpya.Kwa njia ya simu,barua pepe hata kumpigia simu  yule aliyembali nawe.

1.Familia iliyojaa upendo.

Familia itabaki kushikamana hata kama kuna magumu mliyopitia katika mwaka mzima.Unaweza mpa zawadi mzazi wako au hata ndugu walio mbali kama hamuwezi kuwa pamoja wakati wa sikukuu.

2. kushikamana

Licha ya mwaka kuuisha si mwisho wa safari ya maisha ni vema kuendeleea kushirikiana kwa kila jambo mwaka 2017,waweza mtumia ujumbe mtu aliyekuwa nawe bega kwa bega kipindi chote cha mwaka na kumuonyesha kiasi gani alivyoshirikiana nawe na kumtumia salamu ya sikukuu.Wafanyakazi na Wafanyabiashara mnaweza kufanya hivi kwa wateja wenU kwa kuwatumia kadi ,kalenda au chochote ambacho kampuni imeandaa,ili kuimarisha ushirikiano..

3.Upendo.

Katika safari ya mwaka mzima umekutana na watu tofauti waliokupenda na hata waliokutweza lakini huku kata tamaa,basi watakie salamu za sikuuu wale wote waliokuwa karibu nawe pamoja na watu waliokutweza,kwani huwa si vema kulipa ubaya  ,ukifanya hivyo utapata baraka kwa Mungu..Watakie baraka zisizo na kikomo.kuna vitu vingi ambavyo waweza vifanya na vikampa furaha mtu unaye mtakia heri ya sikuku ,aidha Unaweza kuwapa zawadi  au kubuni chochote kitachowafanya wakukumbe hata mwaka unaofuata.


No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu