Enter your keyword

Culture for Life.

Thursday, December 29, 2016

Modeling ni Kazi kama kazi Zingine ." Tidy Clever"

Sinyati blog ilifanikiwa kufanya interview na  Tidy Clever mwanamitindo anayejishughulisha na tasnia  hii ya modeling pia ni msanii wa kuigiza, ameigiza filamu mbili ya Chozi la binti kibena na Songa Mbele.Tidy aliweza kuzungumzia mambo mengi yaliyopo katika tasnia hii ya Modeling.Hivi ndivyo mahojiano yalivyokuwa:

 


JINA KAMILI: Abubakar Athuman

JINA LA KISANII:Tidy Clever

UMRI:23

KABILA:Msukuma

MAKAZI:Arusha.

 Tidy Clever anasema"

"Modeling ni kazi ambayo inanipa heshima,imenifanya kujulikana na watu  na wanatambua nichokifanya.hata kukutana na watu ambao sikutegemea kama ningeweza kukutana nao na kufanya nao kazi.Nimefanya kazi na designer Martn Kadinda,Ally Rehmtullah na kwa sasa nafanya kazi na kampuni ya modeling inaitwa Black fox.

Ni vizuri kama unafanya modeling pia uwe unajishughulisha na kazi zingine kwasababu kazi za modeling ni za msimu.Mimi binafsi nina kampuni yangu ya Filamu ipo maeneo ya Moshono-Arusha."


 CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA TASNIA HII YA  MODELING NCHINI.

Changamoto zipo nyingi ila kubwa ni hizi:

  1. Malipo hafifu yasioendana na mkataba.Wakati mwingine unasaini mkataba wa kufanya kazi na mtu labda n'je ya mkoa,unapofika mfano alikuhaidi utafikia hotelini anakupeleka Guest na wakati mwingine hakupi malipo yako.

  2. Katika jamii ni kwamba modeling inaonekana  kama tasnia ya uhuni.kwamba mtu anayefanya modeling ni shoga,binafsi napenda kuiambia jamii kwamba sikweli ingawa hivyo vitu vipo. kitu cha msingi ni mtu kutambua anachofanya.

Vijana nawashauri kufanya kile kitu anachoweza kufanya na kutosubiri nyumbani ili kuweza kufanya.Vijana wajishughulishe.





 .

 

Designer anayetaka kufanya kazi na mimi kitu cha kwanza lazima aongee na Agency ninayofanya nayo kazi{Black Fox,ipo DSM}.Ila kama ni mimi nimemtafuta tunaongea na kuandikishana mkataba.

Tidy clever katika social Network utampata, facebook kwa jina  la Tidy Clever,Instagram& Twitter, tidyclevertz.Email,tidyclever@hotmail.com

 






No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu